Ticker

6/recent/ticker-posts

KAMPUNI YA DOWEICARE YAWASITIRI WANAFUNZI WA KIKE DODOMA

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amepokea boksi 84 za taulo za kike kutoka kwa kampuni ya DoweiCare ambao ni watengenezaji na wasambazaji wa taulo hizo kwa ajili ya kuratibu ugawaji kwa wanafunzi wa Shule mbalimbali katika Mkoa wa Dodoma.

Akipokea taulo hizo Mhe. Senyamule ameishukuru Kampuni hiyo kwa msaada wa taulo hizo ambazo zinaenda kusaidia watoto wa kike kuwasitiri na kuwezesha kuhudhuria masomo bila kikwazo chochote.

“Ninawashukuru sana kwa kujali makundi yenye uhitaji, ni mchango mkubwa kwa Mkoa wa Dodoma hususan kwa wazazi ambao hawana uwezo wa kuwezesha ununuzi wa taulo za kike. Tutahakikisha tunawapa walengwa ambao ndio wahitaji hasa wenye mazingira magumu.” Senyamule amesisitiza.

Amesema atawasisitiza wanafunzi wanaufaika wa taulo hizo kusoma kwa bidii ili kazi inayofanywa na kampuni ya kusambaza taulo hizo iwe na manufaa na kuonyesha kuwa msingi mkubwa ni wao kupata elimu.

Nae Afisa Taaluma Mkoa wa Dodoma Bi. Jane Mangowi amesema taulo hizo pia zitasaidia wanafunzi wenye makundi maalumu kufikia malengo tarajiwa huku akitoa rai kwa wadau wengine kujitokeza zaidi kusaidia kwakuwa mahitaji bado ni mengi.

Kwa upande wake Afisa Masoko wa Kampuni ya Doweicare Bw. Geoffrey Duma amesema wako tayari kuendea kushirikiana na Ofisi ya Mkuu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na kuchangia taulo zaidi.

Kampuni ya DoweiCare Technology Limited imetoa taulo za kike zenye thamani ya shilingi milioni mbili na laki sita.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akipokea boksi 84 za taulo za kike kutoka kwa kampuni ya DoweiCare ambao ni watengenezaji na wasambazaji wa taulo za kike kwa ajili ya kuratibu ugawaji kwa wanafunzi wa Shule mbalimbali katika Mkoa wa Dodoma. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Bw. Nelson Rumbeli Afisa Afya Mkoa wa Dodoma, Meneja Masoko wa Kampuni ya DoweiCare Bw. Geoffrey Duma na Bi. Jane Mangowi Afisa Elimu – Taaluma Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma.

Maboksi 84 ya taulo za kike zilizotolewa na Kampuni ya Dowei Care kwa ajili ya ugawaji kwa wanafunzi wa kike katika Shule za Dodoma.

Post a Comment

0 Comments