Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI GWAJIMA AZINDUA BARAZA LA TAIFA LA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI


Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima,akizungumza wakati akizindua rasmi Baraza la Taifa la Uwezeshaji wanawake kiuchumi lililofanyika leo Mei 17,2023 jijini Dodoma.


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii ,Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Wakili Amon Mpanju ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wanawake kiuchumi lililofanyika leo Mei 17,2023 jijini Dodoma.


Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Serikali za Mitaa Steven Mutambi,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wanawake kiuchumi lililofanyika leo Mei 17,2023 jijini Dodoma.


Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima (hayupo pichani) wakati akizindua rasmi Baraza la Taifa la Uwezeshaji wanawake kiuchumi lililofanyika leo Mei 17,2023 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini zimehimizwa kuendelea kutoa fursa sawa kwa Wanawake na wanaume kushiriki nafasi za uongozi na maamuzi katika ngazi ya jamii na kuwa sehemu ya maamuzi kwa ustawi wa jamii na Taifa.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima ameyasema hayo Mei 17, 2023 wakati akizindua rasmi Baraza la Taifa la Uwezeshaji wanawake kiuchumi huku akiahidi ushirikiano wa Serikali kwa Baraza hilo katika kumkwamua mwanamke kiuchumi.

Waziri Dkt. Gwajima amewataka viongozi wa Jukwaa hilo kuhakikisha fursa zinazoibuliwa zinawafikia wanawake hasa waliopo vijijini na kuongeza kwamba Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi hali itakayowasaidia kushiriki kwenye nafasi za uongozi.

"Jukwaa hili lihakikishe Wanawake wote wanaona na kupata fursa ya kujiunga na majukwaa yaliopo kuanzia ngazi ya kijiji/Mtaa, Kata, Wilaya hadi Taifa, ili yawawezeshe kupata sehemu ya kujadili mambo yao kuhusu ujasiriamali na biashara kwa ujumla"

Aidha, Dkt. Gwajima pia ametoa wito kwa Halmashauri za Wilaya/ Manispaa na Majiji kuendelea kutenga Fedha za Ndani ili kuwawezesha Wanawake,Vijana na Watu wenye ulemavu kukopa na hatimaye kuweza kujiendeleza kiuchumi.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Serikali za Mitaa Steven Mutambi,amesema wapo tayari kushirikiana na Baraza hilo hasa kwenye fursa za mikopo ambayo Serikali imeshatoa maelekezo ya mikopo yote kupitia benki kuanzia mwaka huu wa fedha.

Mutambi amewapongeza wanawake kwa kuwa mstari wa mbele kurejesha mikopo ya asilimia 10 ikilinganishwa na makundi mengine ambayo yamekuwa yakichechemea kurejesha.

Awali Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Wakili Amon Mpanju amebainisha kwamba mchakato wa uundaji wa Baraza hayo ulianza mwaka 2022 mara baada ya kuzinduliwa kwa Jukwaa la Kizazi chenye usawa bapo uchaguzi wa ngazi ya vijiji hadi mikoa uliendelea na kilicho fanyika leo nikukamilisha mchakato mzima wa kuwa kuwa na Baza la Taifa

"Tupo tayari kutekeleza wajibu wetu hasa jukumu la kisera la kuimarisha na kustawisha majukwaa ya iwezeshaji wanawake kiuchumi kwa kuzingatia miongozo uliotolewa na Wizara" amesema Mpanju.

Akitoa salaam shukrani kwa niaba ya wajumbe wa Baraza hilo, Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Taifa Fatma Kange, amesema wanawake wa Tanzania wanaweza ,kinachotakiwa ni kuelimishwa na kuambiwa kuwa wao ni wajasiriamali.

Post a Comment

0 Comments