Ticker

6/recent/ticker-posts

VIONGOZI WA DINI WAFUNGUKA KWA RC FATMA ,WAMUELEZA WAPI PA KUANZIA.



********************

Na Shemsa Mussa, Kagera .

Mkuu wa mkoa wa Kagera Fatma Mwassa amekutana na viongozi wa madhehebu ya dini mkoani kagera kwa lengo la kuomba ushirikiano katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

Akizungumza na Viongozi hao leo katika ukumbi wa ofisi za Mkoa Mhe Mwassa amesema dhamira yake ni kufanya kazi na kuleta maendeleo ndani ya mkoa na ushirikiano mkubwa unategemea viongozi wa dini.

Amesema,katika shughuli zake za umma anategemea viongozi wa dini kumuweka yeye na Rais Samia katika mikono ya Mungu kwani kazi wanazozifanya zinahitaji hekima,busara na malejereo na ukomavu wa akili, hivyo amesema,viongozi wa dini ndiyo wanaofahamu zaidi Nini Wananchi wanatambua kufanyiwa maendeleo kupitia shughuli zao na kwa waumini wanaowaongoza katika nyumba za ibada.

Nao baadhi ya viongozi hao wa dini akiwema Ndg Haruna kuchwabuta na Fr Samuel Muchunguzi wamesema kuwa ni vema Mkuu wa mkoa kuanza na suala la stend na soko kuwa jambo hilo limekuwa changamoto ya Mkoa kwa muda mrefu .

Aidha wamemuomba Rc Fatma kuupanua mkoa hasa manispaa ya bukoba kwa kupunguza mashamba ya miti na migomba iliyopo ndani ya manispaa na kuwaondoa ngedere wanaoonekana kuzubaa ndani ya mji wa bukoba , pia kuwaondolea ushuru wakulima vijijini ili wawe na uhuru wa mazao yao.

Pia wameongeza kuwa katika suala la maadili ni vema kulipigania somo la dini mashuleni kulithamini somo hilo na kuwepo mitihani ya dini kama mitihani ya masomo mengine na kwa usimamizi bora ili kujenga vizazi vinavyomtegemea na vyenye khofu ya Mungu .

Post a Comment

0 Comments