Meneja wa Kituo cha Warahibu wa Dawa za Kulevya (MAT) wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Tumbi mkoani Pwani Dkt.Victor Noah akitoa maelezo kuhusiana kifaa cha Kieletroniki cha kusajili wa Warahibu wa Dawa za Kulevya pamoja kila moja kuwa na kiwango chake cha Methadone , Kibaha mkoani Pwani.
* Watumiaji wa Dawa za Kulevya wabainika kuwa na maambukizi ya VVU na Ugonjwa wa Ini.
Na Chalila Kibuda, Pwani
Tanzania Health Promotion Support (THPS) kupitia Shirika la Watu wa Marekani CDC wamefanya ziara kituo cha warahibu wa dawa za kulevya (MAT) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Tumbi mkoani Pwani.
Meneja wa Kituo cha Warahibu wa Dawa za Kulevya (MAT) wa Hospitali ya Rufaa ya Tumbi mkoani Pwani Dkt.Victor Noah amesema, kuwa ufadhili wa THPS kupitia Shirika la Marekani CDC umesaidia kutatua changamoto kwa vijana wanaotumia dawa za kulevya wakiwa wamefika kliniki ya MAT wanapata vipimo vya uchunguzi kwa sababu watumiaji hao wanakuwa na magonjwa mengine yaliyotokana na matumizi ya dawa hizo.
Amesema kuwa, vijana waliopata huduma katika kituo hicho ni 428 ambao wote walikuwa na utumiaji wa dawa za kulevya, na walianza dawa lakini baadhi yao wanaacha dawa kwa sababu zao zisizotokana na kituo.
Dkt.Noah amesema kuwa THPS kupitia Shirika la Marekani CDC liko katika kuhakikisha huduma za warahibu wa dawa za kulevya zinapatikana ikiwa ni pamoja na wanaopatikana na virusi vya UKIMWI wanaanza dawa.
Amesema kuwa Warahibu wa dawa za kulevya wanaacha dawa kwa muda wa miaka miwili ndio wanakuwa wako sawa ambapo kituo hicho hadi sasa wanakwenda kuwaachisha methadone vijana 10 na kuendelea na wengine.
Amesema waraibu wa dawa za kulevya 13 walipatikana na Virusi vya UKIMWI ambapo walianzishiwa dawa na maendeleo yao ni mazuri kutokana na ufuatiliaji wa dawa kila moja aliopo kwenye kituo.
Aidha amesema THPS kupitia CDC wametoa Solar kwa ajili ya kituo hicho umeme wa Tanesco unapokatika unatumika umeme wa Solar lengo ni kuhakikisha huduma katika kituo hicho hazisimami kutokana na kukosekana kwa umeme.
Hata hivyo kwa msaada wa THPS katika kituoa cha MAT Kibaha tumeweza kupatiwa Kifaa cha Kieletroniki cha kusajili waraibu wa dawa za kulevya ambapo akiweka alama za vidole kifaa huonyesha picha pamoja na kipimo cha dawa anachotakiwa kupewa.
Dkt.Noah amesema kuwa maji yanayotakiwa kunywa warahibu yanatakiwa kuwa ni maji safi na salama hivyo THPS kupitia CDC waliweka mtambo wa kusafisha maji hayo.
Amesema kuwa Warahibu licha ya baadhi yao kuwa na VVU lakini hupatikana na ugonjwa wa homa ya Ini wakati awali walikuwa hawapimwi homa ya ini lakini sasa wanapata huduma hiyo.
Afisa Ustawi wa Jamii wa MAT Hellen Swai amesema kuwa vijana wanaingia katika matumizi ya dawa za kulevya kutokana na malezi na mkundi ya ujanani.
Amesema mafanikio kwa sasa baada ya Shirika la Marekani CDC kupita THPS vijana wamerekebika na baadhi yao kuoa kutokana na hali zao kutengamaa
Aidha amesema kuwa vijana wameaanzisha mfuko wa wekeza kwa fedha walizokuwa wanatumia kununua dawa za kulevya ambapo wanaweka hadi shilingi milioni moja pamoja na kuwapa mafunzo ya ufundi ambapo walijiunga na kozi ya udereva.
Meneja wa Mradi wa CDC/PEPFAR Afya Hatua wa THPS Dkt.Joshua Mharagi amesemakuwa, vijana wengi wamejitokeza kuanza methadone na kufanya wizi katika mitaa kupungua hayo yakiwa ni sehemu tu ya mafanikio.
Amesema vijana wameanzisha vikundi vya uzalishaji hali ambapo jamii inatakiwa kuwakubali kwani wanaweza kutokana na mafunzo mbalimbali ndani ya kituo cha MAT.
Afisa Ustawi wa MAT Kibaha Hellen Swai akionesha jinsi warahibu wa dawa za kulevya wanavyowekeza fedha zao ambazo walikuwa wananulia dawa za kulevya MAT Kibaha mkoani mkoani Pwani.
Mrahibu wa Dawa za Kulevya Deborah Lema akijiandaa kwenda kunywa methadone katika Kituo cha MAT, Kibaha mkoani Pwani.
Meneja wa Kituo cha Warahibu wa Dawa za Kulevya (MAT) wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Tumbi mkoani Pwani Dkt.Victor Noah akionesha mtambo wa kusafisha maji ikiwa ni ufadhili wa THPS kuptia Shirika la Marekani CDC katika Kituo cha MAT Kibaha mkoani Pwani.
Meneja wa Kituo cha Warahibu wa Dawa za Kulevya (MAT) wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Tumbi mkoani Pwani Dkt.Victor Noah akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ufadhili wa THPS kuptia Shirika la Marekani CDC katika Kituo cha MAT Kibaha kwa kuweka Solar kuondoa changamoto ya umeme wa Tanesco , mkoani Pwani.
Meneja wa Kituo cha Warahibu wa Dawa za Kulevya (MAT) wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Tumbi mkoani Pwani Dkt.Victor Noah akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ufadhili wa THPS kuptia Shirika la Marekani CDC katika Kituo cha MAT Kibaha , mkoani Pwani.
0 Comments