Jeshi la Polisi Mkoani songwe limefanikiwa kukamata mabunda 50 ya sigara ambayo ni packet 500 zenye uzito wa kilo Nane ambazo zimetengenezwa kwa kutumia bangI ambazo zilizokuwa zikisafirishwa kutoka nchi ya Zimbabwe na kuingizwa nchini Tanzania.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, ACP Theopista Mallya amethibitisha kukamatwa kwa madawa hayo ya kulevya aina ya bangi tukio ambalo lilitokea April 29 Mwaka huu katika Mpaka wa Tunduma.
Aidha Kamanda Mallya ameongeza kwa kusema kuwa mzigo huo ulikuwa ukisafirishwa kwa kutumia basi la abiria la Kampuni ya Classic lenye namba za usajili za nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo 6321AA25 ambalo lilikuwa likitokea nchini Zimbwabwe kwenda jijini Dar es Salaam ambapo mabunda hayo yalikuwa yamefichwa nyuma ya kiti cha dereva.
0 Comments