Ticker

6/recent/ticker-posts

SHULE YA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM YA BUHANGIJA YAPATA MSAADA WA DOLA 10,000 KUTOKA SHIRIKA LA NVeP KWA UFADHILI WA BARRICK


Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu,Cheick Sangare (wa pili kutoka kulia),akimkabidhi msaada wa hundi ya dola 10,000 kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi ya watoto wenye mahitaji maalum ya Buhangija iliyopo katika manispaa ya shinyanga,Fatuma Gilalah (wa nne kutoka kulia) na Afisa elimu ya msingi,Mary Maka (wa tatu kutoka kushoto mwenye miwani) . Msaada huo umetokana na sehemu ya fedha zilizotolewa na taasisi ya Nos Vies en Partage (NVeP), inayofadhiliwa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow.Wengine pichani ni wafanyakazi wa Barrick na wawakilishi wa wanafunzi wa shule hiyo.Hafla ya kukabidhi msaada huo ilifanyika katika mgodi wa Bulyanhulu.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Cheick Sangare (wa pili kutoka kulia), akimkabidhi msaada wa hundi ya dola 10,000 kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi ya watoto wenye mahitaji maalum ya Buhangija iliyopo katika manispaa ya shinyanga,Fatuma Gilalah na Afisa elimu ya msingi,Mary Maka ( mwenye miwani) .Msaada huo umetokana na sehemu ya fedha zilizotolewa na taasisi ya Nos Vies en Partage (NVeP), inayofadhiliwa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow.Wengine pichani ni wafanyakazi wa Barrick.
Afisa Mwandamizi wa Mahusiano ya Jamii wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu akitoa utambulisho kwa wageni wakati wa hafla hiyo.
Meneja Mkuu wa Barrick Bulyanhulu,Cheick Sangare akiwa na Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Buhangija, Fatuma Gilalah na Afisa Elimu ya Msingi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga,Mary Maka (Kushoto)
Baadhi ya wanafunzi wanaosoma katika shule ya Buhangija pia walihudhuria katika hafla hiyo.
***

Shirika la ya Nos Vies en Partage (NVeP) kwa kushirikiana na kampuni ya Barrick,wametoa msaada wa dola za Kimarekani 10,000 kwa shule ya msingi ya watoto wenye mahitaji maalum ya Buhangija iliyopo mkoani Shinyanga kwa ajili ya kuboresha mazingira ya kusomea ya wanafunzi wa shule hiyo.



Msaada huo umetokana na sehemu ya fedha zilizotolewa na taasisi ya Nos Vies en Partage (NVeP), iliyoanzishwa na inayofadhiliwa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow, kwa ajili ya kusaidia makundi maalum kama vile Wanawake,watoto na makundi mengine yenye uhitaji yasiofaidika na ukuaji wa kiuchumi barani Afrika.



Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika katika Mgodi wa Bulyanhulu wilayani Msalala, Meneja Mkuu wa Mgodi huo,Cheick Sangare, alisema kila robo ya mwaka,taasisi imeweza kutoa misaada yenye tija na manufaa ya moja kwa moja kwenye jamii zenye uhitaji.



"Hadi sasa tumeweza kutoa msaada kwa zaidi ya mashirika 10 nchini Tanzania kupitia taasisi ya NVeP, leo tuko hapa kuleta mabadiliko kwa shule ya msingi Buhangija ambayo inatoa elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum kwa kuipatia msaada wa dola za kimarekani 10, kwa ajili ya kuboresha mazingira ya wanafunzi kupata elimu", alisema Sangare.

Akiongea baada ya kupokea hundi ya fedha za msaada huo, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Fatuma Gilalah, aliyeongozana na na Afisa Elimu ya Msingi wa Manispaa ya Shinyanga Mary Maka, alishukuru  kwa msaada huo ambao alisema kuwa utasaidia kutatua changamoto mbalimbali kwa ajili ya kuboresha mazingira ya wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo.

Alisema pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali kuboresha mazingira ya kuwapatia elimu watoto wenye mahitaji maalum wanaosoma katika shule hiyo bado kuna changamoto mbalimbali kwa upande wa miondombinu na vifaa vya kufundishia.

“Tunashukuru kwa msaada huu tuliopokea siku ya leo kutoka Barrick na utasaidia kuboresha mazingira ya kusomea ya wanafunzi wetu”, alisema Gilalah.

Alisema shule hiyo inatoa elimu elimu kwa wanafunzi wenye ulemevu wa ngozi (wenye ualbino), wasioona na wenye usikivu hafifu vizuri (viziwi).


Post a Comment

0 Comments