NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
KATIKA kipindi cha miaka miwili, Shirika la Posta Tanzania limefanikiwa kutoa huduma za posta ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kutosheleza mahitaji ya kitaifa ya huduma za usafirishaji, biashara ya mtandao, Vituo vya Huduma za Kiserikali na Miamala ya kifedha ndani ya Nchi.
Amayesema hayo leo Mei 1,2023 Jijini Dar es Salaam Kaimu Meneja Mkuu wa Rasilimali za Shirika la Posta Tanzania, Bw.Aron Oyye wakati akisoma hotuba kwa niaba ya Postamasta Mkuu katika kuadhimisha Sikukuu ya Wafanyakazi Mei Mosi.
Amesema miongoni mwa mafanikio ambayo waameyapata mpaka sasa ni pamoja na kutengeneza Mfumo wa Posta Kiganjani na kufanikiwa kuuzindua ili uweze kutumika katika kutoa huduma.
Aidha amesema Katika kuendelea kuimarisha vitendea kazi Shirika limenunua magari ya usambazaji (delivery vans) matatu (3) na magari mawili (2) ya viongozi.
Amesema Kwa kupitia Serikalini Shirika limefanikiwa kupata fedha za Ujenzi wa jengo la ofisi ya Makao Makuu Jijini Dodoma, jengo ambalo linatarajiwa kugharimu zaidi Shilingi Bilioni Ishirini za Kitanzania.
Hata hivyo amesema Shirika limefanikiwa kupata Fedha kutoka Serikalini Kiasi cha Shilingi Bilioni Nane za Kitanzania, fedha ambazo zitatumiwa katika kuimarisha vitendea kazi na kuimarisha mifumo ya TEHAMA.
Vilevile amesema Shirika la Posta Tanzania litaendelea kufanya juhudi za kutatua changamoto zilizopo na kuboresha mazingira ya kazi kwa kuhakikisha vitendea kazi vinapatikana pamoja na Stahiki za watumishi zinapatikana na kutolewa kwa wakati.
"Sambamba na kutambua mchango mkubwa wa rasilimali watu na kuongeza morali ya kazi, tutakuwa na upandishaji wa vyeo (Promotion) na ubadilishaji wa kada (Recategorisation) kwa mwaka 2022/2023 kwa vigezo husika". Amesema






(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
0 Comments