Na Crispin Gerald
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amosi Makala ameitaka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kuongeza nguvu katika uzalishaji wa maji kupitia visima virefu vya Kigamboni na maeneo mengine pembezoni mwa Jiji ili viweze kuongeza upatikanaji wa maji na kukidhi mahitaji ya wananchi hususani kipindi cha kiangazi.
Ameyasema hayo wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya uchimbaji na usafishaji wa visima virefu vya Kigamboni vinavyochimbwa na kusafishwa ili kuongeza huduma.
Amebainisha kuwa kuna kila haja kwa DAWASA kuhakikisha visima virefu vinavyotakiwa kuchimbwa vinachimbwa kwa haraka na vile vinavyotakiwa kusafishwa kazi ifanyike hivyo kwa kuwa vitasaidia katika upatikanaji wa maji wakati wa kiangazi.
Amemtaka Mkandarasi wa kampuni ya Serengeti kurejea kazini mara moja ili akamilishe kazi ya uchimbaji wa visima pamoja na kusafisha vilivyopo.
"Leo nimekuja rasmi kuona maendeleo ya mradi wa visima na kujua mpango uliopo wa kuhakikisha visima vyote 20 vinakamilika na vinatoa maji sambamba na maelekezo ya Mhe. Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa aliyoyatoa wakati wa ziara yake Kigamboni," ameeleza.
"Tunahitaji kuwa na maji ya kutosha ya kuweza kuhudumia wananchi wote wa Kigamboni, katikati ya Jiji na maeneo ya pembezoni hususani wakati wa kiangazi," amesema Mhe. Makala.
Amebainisha kuwa visima saba vinavyotoa maji kwa sasa havitoshi kuweza kuhudumia wananchi wote, inahitajika nguvu zaidi ya kuongeza visima ili wakati wa kiangazi pasiwe na changamoto ya wakati uliopita.
Ameitaka Menejimenti ya Mamlaka kuandaa mpango kazi wa ujenzi wa miundombinu ya kupokea maji kutoka kwenye visima virefu na kuyapeleka kwenye bomba kuu.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe Halima Bulembo ameahidi kufanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa na Mhe. Mkuu wa Mkoa kuhusu kuhakikisha huduma ya maji inaimarika kwenye maeneo yote.
"Tutahakikisha kazi hii inatekelezwa mara moja ili wananchi wa eneo hili la Kigamboni ambao hawajapata maji kwa muda mrefu wapate maji," amesisitiza.
Akielezea utekelezaji wa mradi huu Mwakilishi wa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Shabani Mkwanywe amesema Mamlaka imepokea maelekezo yote toka kwa Mhe. Mkuu wa Mkoa na kwamba utekelezaji wake utaanza mara moja.
Amesema kuwa tayari Mamlaka imeandaa mpango kazi wa namna ya kuongeza uzalishaji wa maji kupitia visima virefu vya Kigamboni pamoja na maeneo mengine ili kuongeza upatikanaji wa maji pamoja na kukabiliana na changamoto wakati wa kiangazi.
"Kwa maeneo haya ya Kigamboni, kazi kubwa ya kuunganisha wananchi na huduma ya majisafi inaendelea kwenye mitaa mbalimbali," ameeleza.
Mhe. Mkuu wa Mkoa ametembelea maendeleo ya mradi wa visima virefu pamoja na kituo cha kusukuma maji kwenda kwenye tenki kubwa la lita milioni 15,

0 Comments