Ticker

6/recent/ticker-posts

RC FATMA AKUTANA WA WAKUU WA TAASISI ZA UMMA MKOA WA KAGERA


Mkuu wa Mkoa wa Kagera Bi Fatma Mwassa akizungumza  wakati wa kikao chake na wakuu wa taasisi za serikali kwa lengo la kuzifahamu na kuzijua zaidi changamoto katika idara hizo.


**********************

Na Shemsa Mussa, kagera

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Bi Fatma Mwassa amekutana leo na kuzungumza na wakuu wa taasisi za serikali kwa lengo la kuzifahamu na kuzijua zaidi changamoto katika idara hizo

Amesema hatokuwa tayari kuwavumilia Watendaji Wazembe, wavivu,wacheleweshaji wa miradi ya Maendeleo, waongo wabadhilifu wa mali za umma kuwa hatokuwa tayari kutoka kwa watumishi watakaoonekana kukwamisha Maendeleo huku akiahidi kutotumia hata dakika moja kuwasamehe pindi wakifanya uzembe.

"Tutakukataa mara moja wewe mtumishi utakayeonesha uzembe katika kazi na tutaleta wanaotufaa hivyo ni lazima mkafanye au ufanye mabadiliko ya haraka kabla ya kukubaini" alisema Fatma.

Amesema anahitaji kuona Mkoa huo unatoka katika nafasi ya sasa kuichumi na kupanda juu huku akitegemea watumishi hao kufanya ubunifu wa haraka katika miradi mikubwa ya Maendeleo.

aidha ameahidi kuhakikisha anaanza na miradi sugu iliyoonekana kukwama kwa muda mrefu ikiwemo ujenzi wa Stendi na Soko ambapo pia

amewakumbusha watumishi hao wajibu wao ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa bidii ili maendeleo ya Mkoa huo yaonekane kwa haraka.

Hata hivyo jumla ya Taasisi 15 zimewasilisha taarifa za vitengo vyao na kubainisha changamoto katika utendaji wake ambapo Mkuu huyo wa Mkoa ameahidi kuanza kuzitatua mara moja.

Post a Comment

0 Comments