Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS DKT. MWINYI AZINDUA KAMATI YA MARIDHIANO KATI YA CCM NA ACT -WAZALENDO IKULU ZANZIBARG

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wa Chama cha ACT-Wazalendo, wakati akizindua Kamati ya Maridhiano Kati ya CCM na ACT –Wazalendo, uzinduzi huo uliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 31-5-2023, na (kulia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla na (kushoto kwa Rais) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya na Wajumbe wa Kamati ya Maridhiano Kati ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha ACT-Wazalendo, baada ya kuizindua kamati hiyo leo katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar na (kulia kwa Rais)Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ambae pia ni Makamu Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Mhe. Othman Masoud Othman na Naibu Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo Mhe. Nossor Ahmed Mazrui na (kushoto kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambae ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Hemed Suleiman Abdulla na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Mohammed Said Dimwa.(Picha na Ikulu)

Post a Comment

0 Comments