RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiondoa pazia kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ufunguzi wa Msikiti Mkuu wa Paje Wilaya ya Kusini Unguja (kushoto) Mfadhili wa ujenzi wa Msikiti huu Dkt. Mahir Bakar,hafla hiyo ya ufunguzi wa msikiti huo uliyofanyika leo 12-5-2023 na kujumuika na Wananchi wa Paje katika Ibada ya Sala ya Ijumaa, baada ya ufunguzi wake.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kuufungua Msikiti Mkuu wa Paje Wilaya ya Kusini Unguja leo 12-5-2023, na (kulia kwa Rais) Mfadhili wa Ujenzi wa Msikiti huo Dkt. Mahir Bakar na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Hadid Rashid Hadid.(Picha na Ikulu)
MUONEKANO wa Msikiti Mkuu wa Paje Wilaya ya Kusini Unguja uliofunguliwa leo 12-5-2023 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi, na kujumuika na Wananchi wa Paje katika Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika msikiti huo baada ya ufubguzi wake.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuwasalimia Wananchi wa Paje Wilaya ya Kusini Unguja baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Msikiti huo baada ya kufunguliwa leo 12-5-2023.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Wananchi wa Paje kuitikia dua ikisomwa na Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume, baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Msikiti Mkuu wa Paje Wilaya ya Kusini Unguja na (kushoto kwa Rais) Mfadhili wa Ujenzi wa Msikiti huo Dkt. Mahir Bakar na (kulia kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar.Mhe. Haroun Ali Suleiman na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Hadid Rashid Hadid.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwasalimia Watoto wa Paje Wilaya ya Kusini Unguja baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Msikiti Mkuu wa Paje leo 12-5-2023, baada ya kuufungu na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Hadid Rashid Hadid .(Picha na Ikulu)
0 Comments