Ticker

6/recent/ticker-posts

MKENDA AKITAKA CHUO CHA ST.JOHN KUENDELEA KUPANUA ZAIDI UWEZO WA KUDAHILI

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akizungumza wakati akisoma hotuba akishamwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango katika uzinduzi wa jengo la utawala la Chuo Kikuu cha Mtakatifu John uliofanyika leo Mei 26,2023 Jijini Dodoma
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akiwa pamoja na Mhashamu Baba Askofu Mkuu, Kanisa Aglikana Tanzania Dkt.Maimbo Mndolwa wakifunua pazia kuzindua jengo la utawala la Chuo Kikuu cha Mtakatifu John.leo Mei 26,2023 Jijini Dodoma.

*****************

Serikali imesema itaendelea kuunga mkono vyuo vikuu vinavyomilikiwa na taasisi za Dini na sekta binafsi kwa sababu vinachangia kutoa huduma ya elimu kwa watanzania.


Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda Mei 26, 2023 jijini Dodoma akimwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango katika uzinduzi wa jengo la utawala la Chuo Kikuu cha Mtakatifu John.


Kiongozi huyo ameongeza kuwa katika kutekeleza hilo, Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliagiza zitengwe fedha katika Mradi wa HEET kwa ajili ya kufadhili masomo ya wahadhiri walioajiriwa kwenye vyuo vikuu binafsi ikiwa ni pamoja na vyuo vikuu vinavyomilikiwa na taasisi za dini.


"Katika kutekeleza agizo la Rais wetu tumetenga jumla ya dola za kimarekani milioni moja kwa ajili ya kufadhilia masomo ya wahadhiri kutoka Vyuo Vikuu Binafsi katika Shahada za Uzamili na Uzamivu" amesisitiza kiongozi huyo


Prof. Mkenda ameongeza kuwa mpaka sasa wahadhiri 27 wa vyuo vikuu binafsi wamenufaika na ufadhili huo, huku Chuo Kikuu cha Mtakatifu John nacho kikinufaika ambapo wahadhiri wake watatu wanasomeshwa katika ngazi Shahada za Uzamivu nje ya nchi.


Waziri Mkenda amekitaka Chuo Kikuu cha Mtakatifu John kuendelea kupanua zaidi uwezo wa kudahili kwa kuimarisha ubora wa mafunzo na kuongeza miundombinu ya chuo.


Aidha, amevitaka vyuo vikuu vyote nchini kuhakikisha vinasimamia ubora wa elimu inayotolewa ili kuzalisha wataalamu mahiri wenye weledi na kuwataka Wahadhiri kujikita katika kufanya utafiti.


Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Yohana Msanjila amesema kuwa Chuo hicho kilikuwa na changamoto ya ofisi kwa watumishi na kupelekea wanataaluma ambao ni wakuu wa idara kuchangia ofisi kinyume na taratibu za usimamizi wa vyuo vikuu, hivyo changamoto hiyo ndo iliyotoa msukumo wa kufikia uamuzi wa kujenga jengo hilo la utawala


Prof. Msanjila ameongeza kuwa jengo hilo lenye vyumba vya ofisi 33, kumbi za mikutano mbili, sehemu za kupumzikia tatu na jiko limegharimu zaidi ya shilingi bilioni moja na miliioni mia tisa mpaka kukamilika kwake.


Naye Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha St. John's Prof. Penina Mlama amesema chuo hicho kimekuwa na mchango mkubwa katika kutoa elimu ambapo mpaka kimeshatoa wahitimu 10002


Prof. Mlama amemhakikisha Waziri Mkenda kuwa chuo hicho kitaendelea kutoa mchango kwa taifa kwa kuandaa wataalamu katika fani mbalimbali.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akiwa pamoja na Mhashamu Baba Askofu Mkuu, Kanisa Aglikana Tanzania Dkt.Maimbo Mndolwa wakipongezana mara baada ys uzinduzi wa jengo la utawala la Chuo Kikuu cha Mtakatifu John.leo Mei 26,2023 Jijini Dodoma.


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati akisoma hotuba akishamwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango katika uzinduzi wa jengo la utawala la Chuo Kikuu cha Mtakatifu John uliofanyika leo Mei 26,2023 Jijini Dodoma
Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu John, Donald Mtetemela akizungumza katika uzinduzi wa jengo la utawala la Chuo Kikuu cha Mtakatifu John uliofanyika leo Mei 26,2023 Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Mtakatifu John, Prof. Penina Mlama akizungumza katika uzinduzi wa jengo la utawala la Chuo Kikuu cha Mtakatifu John uliofanyika leo Mei 26,2023 Jijini Dodoma.

Makamu Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu John, Prof.Yohana Msanjila akisoma hotuba katika uzinduzi wa jengo la utawala la Chuo Kikuu cha Mtakatifu John uliofanyika leo Mei 26,2023 Jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akisalimiana na Mhashamu Baba Askofu Mkuu, Kanisa Aglikana Tanzania Dkt.Maimbo Mndolwa baada ya kuwasili katika uzinduzi wa jengo la utawala la Chuo Kikuu cha Mtakatifu John uliofanyika leo Mei 26,2023 Jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akisalimiana na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Mtakatifu John, Prof. Penina Mlama baada ya kuwasili katika uzinduzi wa jengo la utawala la Chuo Kikuu cha Mtakatifu John uliofanyika leo Mei 26,2023 Jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akisalimiana na Makamu Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu John, Prof.Yohana Msanjila baada ya kuwasili katika uzinduzi wa jengo la utawala la Chuo Kikuu cha Mtakatifu John uliofanyika leo Mei 26,2023 Jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika uzinduzi wa jengo la utawala la Chuo Kikuu cha Mtakatifu John uliofanyika leo Mei 26,2023 Jijini Dodoma
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akipokea zawadi ya picha kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango kwenye hafla ya uzinduzi wa jengo la utawala la Chuo Kikuu cha Mtakatifu John uliofanyika leo Mei 26,2023 Jijini Dodoma
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akipokea zawadi kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu John kwenye hafla ya uzinduzi wa jengo la utawala la Chuo Kikuu cha Mtakatifu John uliofanyika leo Mei 26,2023 Jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Mtakatifu John, Prof. Penina Mlama wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo la utawala la Chuo Kikuu cha Mtakatifu John uliofanyika leo Mei 26,2023 Jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa jengo la utawala la Chuo Kikuu cha Mtakatifu John uliofanyika leo Mei 26,2023 Jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu John katika hafla ya uzinduzi wa jengo la utawala la Chuo Kikuu cha Mtakatifu John uliofanyika leo Mei 26,2023 Jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akiwa kwenye picha ya pamoja na wakurugenzi wa taasisi za Elimu nchini katika hafla ya uzinduzi wa jengo la utawala la Chuo Kikuu cha Mtakatifu John uliofanyika leo Mei 26,2023 Jijini Dodoma.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Post a Comment

0 Comments