Ticker

6/recent/ticker-posts

MAWAKALA, WANAHABARI MASHUHURI KUTOKA CHINA WATEMBELEA TANZANIA KUFANYA "ROYAL TOUR." MCHENGERWA AWAPOKEA.


Na John Mapepele

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mohamed Mchengerwa amewaongoza watanzania kuwapokea wawakilishi wa makampuni makubwa duniani ya mawakala wa utalii kutoka China wakiwa wameongozana na Vyombo vya Habari vikubwa.

Akizungumza mara baada ya kuwapokea wageni hao wapatao 40 katika uwanja wa ndege wa Arusha leo Mei 17, 2023 alipoambatana na Naibu Katibu Mkuu, Anderson Mutatembwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Taanzania (TTB), Damasi Mfugale amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada alizozifanya kutaitangaza Tanzania kupitia Filamu ya The Royal Tour.
Aidha, ametoa wito kwa watanzania kuja kuwekeza katika sekta utalii hususan kwenye ujenzi wa mahoteli kwa kuwa katika kipindi hiki idadi ya watalii imeongezeka ukilinganisha na nyakati nyingine zilizopita.

Ujumbe wa Mawakala hao na Waandishi wa Habari unatarajia kufanya mkutano maalum wa kibiashara na wadau mbalimbali wa utalii ili kujadili na kufanya biashara za utalii ambapo Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mohamed Mchengerwa anatarajia kuwa mgeni rasmi na baadaye watatembelea Hifadhi mbalimbali za watalii.

Naye, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Anderson Mutatembwa amesema Wizara inatarajia kutoa mwongozo wa fursa za uwekezaji ikiwa ni jitihada za Serikali katika kuboresha sekta ya utalii hapa nchini.Uratibu wa ziara hii ya mafunzo umefanywa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii, ikishirikiana na wadau wa utalii, Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Ubalozi wa Tanzania nchini China, Benki ya NMB na Shirika la Ndege la Tanzania.



Post a Comment

0 Comments