NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Serikali inakusudia kuhakikisha Watanzania wananufaika na rasilimali za taifa kwa kuboresha mfumo wa elimu, afya na huduma za kijamii kwa watanzania wote.
Hivyo basi, tunapaswa kuhakikisha kwamba tunakuwa na uchumi jumuishi na shindanishi utakaolenga kuboresha hali ya maisha ya watanzania wote na yote yatawezekana ikiwa tutafanya tafiti na bunifu za kutosha zinazotoa masuluhisho ya changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii.
Ameyasema hayo Mei 23,2023 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt.Amos Nungu wakati akimuwakilisha Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda Kufungua Maonesho ya Nane ya Tafiti na Ubunifu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Alisema Katika maonesho hayo, jamii ya Watanzania itafaidika kutokana na matokeo ya tafiti zinazofanywa na wataalamu wa vyuo vikuu na hivyo kuvisogeza vyuo hivyo karibu zaidi na jamii.
"Ninatoa wito kwa vyuo vikuu vingine nchini Tanzania kuzingatia kwamba utaratibu wa kufanya utafiti na kisha kuonesha matokeo tafiti kama mnavyofanya ninyi kutaimarisha uhusiano wa karibu baina ya vyuo na soko la ajira". Alisema
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye alisema kwa kutambua umuhimu wa tafiti na ubunifu katika kutatua changamoto zinazoikabili jamii ya Watanzania na Taifa kwa ujumla, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimekuwa kikitenga bajeti kwa kutegemea vyanzo vya ndani. Katika mwaka wa fedha 2022/2023, UDSM imetenga kiasi cha TZS 3,150,000,000 kwa ajili ya kufadhili wanataaluma ili wafanye tafiti na bunifu mbalimbali. Ambapo, kiasi cha TZS 2,450,000,000 ni kwa ajili ya utafiti na kiasi cha TZS 700,000,000 kwa ajili ya ubunifu.
"Jumla ya miradi 92 ilishinda ambapo miradi 88 ni ya utafiti na miradi 4 ni ya ubunifu. Pesa zote hizi ziligawiwa kwa wanataaluma waliowasilisha mapendekezo ya utafiti na miradi mbalimbali ya ubunifu". Alisema
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye akizungumza katika ufunguzi wa Maonesho ya Nane ya Tafiti na Ubunifu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam uliofanyika leo Mei 23,2023 Jijini Dar es Salaam
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye akizungumza katika ufunguzi wa Maonesho ya Nane ya Tafiti na Ubunifu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam uliofanyika leo Mei 23,2023 Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt.Amos Nungu akizungumza wakati akimuwakilisha Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda Kufungua Maonesho ya Nane ya Tafiti na Ubunifu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam uliofanyika leo Mei 23,2023 Jijini Dar es Salaam
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam - Utafiti, Prof. Nelson Boniface akizungumza katika ufunguzi wa Maonesho ya Nane ya Tafiti na Ubunifu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam uliofanyika leo Mei 23,2023 Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya wadau wa Utafiti na Ubunifu wakiwa katika ufunguzi wa Maonesho ya Nane ya Tafiti na Ubunifu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam uliofanyika leo Mei 23,2023 Jijini Dar es Salaam
0 Comments