Mwakilishi wa Mganga Mkuu ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Afya ya Uzazi Mama na Mtoto kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Ahmad Makuwani akizungumza katika mkutano uliowakutanisha watafiti na wadau mbalimbali wa sekta ya afya Jijini Dar es salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Afya Ifikara, Dk. Honorati Masanja akizungumza katika mkutano uliowakutanisha watafiti na wadau mbalimbali wa sekta ya afya Jijini Dar es salaam
**********************
Na Magrethy Katengu
Wakati Tanzania ikipambana kuhakikisha Janga la Ugonjwa Malaria unatokomezwa kabisa lakini imebainika kuwa changamoto kubwa inayokwamisha juhudi zisikamilike ni pamoja na matokeo ya tafiti mbalimbali zinazofanyika kushindwa kuwafikia walengwa na kuonesha baadhi ya mikoa hali ya malaria bado iko juu ikiwemo Mtwara, Shinyanga, Kagera kwa asilimia 15-20
Akizungumza jijini Dar es Salaam Mwakilishi wa Mganga Mkuu ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Afya ya Uzazi Mama na Mtoto kutoka Wizara ya Afya, Dk. Ahmad Makuwani katika mkutano uliowakutanisha watafiti na wadau mbalimbali wa sekta ya afya ukiwa na lengo la kujadili masuala ya Afya hususano namna ya kusaidia kutomeza malaria nchini ifikapo mwaka 2030 ugonjwa huo uwe umetokomezwa kabisa.
“Tunafanya tafiti nyingi za masuala ya afya na mara nyingi tafiti haziwafikii walengwa na hawajii namna gani wanaweza kuyatumia matokeo kwani kuna mikoa tumefanikiwa kupunguza hadi kufikia kiwango cha malaria asilimia moja ni ikiwemo Kilimanjaro Arusha hivyo kupitia mkutano huu utasaidia kupata suluhisho la kusaidia mikoa ambayo kiwango chake kiko juu" amesema Dkt
Sanjari na hayo Dkt amesema inahitajika mikakati mikubwa ili kuweza kutokomeza Malaria kwani imekiwa ikisababisha vifo vingi vya Watoto na Watu wazima kwa haraka hivyo kila mmoja wetu hapa ni shahidi kwamba tunahitaji kutokomeza ugonjwa huu ifikapo mwaka 2030
Amesema watafiti hao wanajiuliza maswali kwa nini mikoa kama Arusha, Manyara, Kilimanjaro na mingine imefikisha asilimia moja kupunguza malaria na kwa nini imekuwa changamoto kwa mikoa mingine ambayo bado ina viwango vya juu vya ugonjwa huo hatari.
Hata hivyo amefafanua kuwa hali ya ungonjwa wa malaria siyo nzuri kuna mikoa bado ipo kwenye asilimia 15 hadi 20 ambayo ni Kanda ya Ziwa na Pwani na bado ugonjwa huo unaua watoto wenye umri chini ya miaka mitano.
“Wenzetu Zanzibar wamefanikiwa kutomeza malaria bado bara, watafiti wanaumiza kichwa kwenye mkutano huu kutafuta majibu yatakayo tusaidia kupata mwarobaini na uwezo wa kutokomeza ugonjwa wa malaria ifakapo mwaka 2030,” amesisitiza Dk. Makuwani.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Afya Ifikara, Dk. Honorati Masanja amesema sababu zinazosababisha ongezeko la maralia nchini ni tabia za watu kutokuhudhuria hospitali kwa wakati pindi wanapopata malaria.
Amesema badala yake wanajitibu kienyeji hali inayosababisha vijidudu vya malaria kuongezeka na kusababisha madhara makubwa kwa mgonjwa wakati mwingine kupelekea kifo.
“Kuna sababu nyingi zinazosababisha ongezeko la malaria kwa baadhi ya mikoa ikiwa ni pamoja na tabia za watu na hizi afua za maralia kutowafikia walengwa kwa wakati,”amesema Dk. Masanja.
Naye Mwakilishi kutokomeza Malaria Zanzibar, Safia Mohamed Ali amesema Zanzibar imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutokomeza ugonjwa huo sababu idadi ya watu Nzanzibar ni ndogo ukolinganisha na Bara hivyo kwa vile kisiwa inafanikishwa kwa urahisi kutoa elimu jumuishi ya kugawa vyandarua kwa kila kaya
"Ukichukulia afua ya kutokomeza Malaria 1969 Shirika la Afya Duniani WHO walitangazia Zanzibari imetokeza kabisa Malaria kutokana na jamii ya wakati ule hatuwezi kusema kusema ilitokomea lakini mwaka 1980 iliridi tena jitihada zilifanyika kuleta neti kwa wamama wajawazito pamoja na Watoto na kufika 2006 upigaji Dawa ulichangia kutokomeza tena ukiangalia kwa bara walichelewa hatua hii matumizi ya dawa 2003 pamoja na ugawaji wa Dawa tanaendelea na mikakati hiyo mpaka Sasa" Amesema Safia
Kwa upande wake Mwakilishi wa Bunge kwenye mkutano huo, Dk. Hamis Kigwangalla amesema Bunge kwa nafasi yao wataishauri Serikali kutumia mbinu ambazo zitasaidia kutokomeza maralia kwani lengo kufikia zero malaria ifikapo 2030 ikiwemo kuweka sera mathubuti
Aidha, Kigwangala ameongeza kuwa Zanzibar imefanikiwa kutokomeza malaria kwani wao walijikita moja kwa moja kwenye kutokomeza wakati bara walijitika kwenye kudhibiti hali iliyosababisha mafanikio makubwa wa Zanzibar.
Naye Mjumbe wa Baraza la kutokomeza Malaria Zuena Mohamedi Msanii wa muziki maarufu Shilole amesema ana jukumu kibwa la kutoa hamasa kuanzia vijijini na mijini kutoa hamasa kwa jamii namna ya kujikinga na Malaria ikiwemo kutoa elimu Usafi majumbani, kutumia dawa za kuua mzalia ya mbu, na matumizi ya chandarua ataanzia katika mikoa ambayo kiwango cha malaria kiko juu.
0 Comments