Chuo cha Ustawi wa Jamii kinashiriki katika maonesho ya vyuo vya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi (NACTVET) yanayofanyika katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid Karume Jijini Arusha kuanzia tarehe 16 Mei 2023 ambayo yatadumu mpaka tarehe 22 Mei 2023.
Katika maonesho hayo Chuo cha Ustawi wa Jamii kimepata fursa ya kuelezea kozi mbalimbali zinazotolewa na Chuo, kutoa huduma ya usajili wa wanafunzi pamoja na kutoa elimu, ushauri, na msaada wa kisaikolojia (bure) kwa watu mbalimbali waliotembelea katika banda la Chuo.
0 Comments