Ticker

6/recent/ticker-posts

HISTORIA MPYA YAANDIKWA TANZANIA, UZINDUZI WA IKULU CHAMWINO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Mei 20, 2023 ameandika historia mpya ya Tanzania kwa kuzindua Majengo mapya ya Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma akishuhudiwa na mamia ya watanzania pamoja na wageni mbalimbali kutoka nje ya Tanzania.

Katika hafla za uzinduzi huo Rais, Dkt. Samia alisema jambo hilo ni la kihistoria kwa watanzania kwani kwa mara ya kwanza, wameweza kujenga Ikulu yao kwa kutumia rasilimali zao pamoja na wataalamu wa ndani ambapo alisema kukamilika kwa mradi huo ni jitihada za Serikali za Awamu zote Sita za uongozi aidha, Rais Samia alisema aliahidi kukamilisha miradi aliyoipokea kutoka kwa mtangulizi wake Hayati Dkt. John Magufuli, hivyo kukamilika kwa mradi huu ni utekelezaji wa kauli yake.

“Nilipokabidhiwa hatamu za kuiongoza nchi yetu, niliahidi nitaendeleza mema yaliyopo, nitaboresha inapobidi na nitaleta mema mapya, ujenzi wa Ikulu hii ni moja ya miradi niliyorithi kutoka kwa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli na ni mradi wa pili kuukamilisha, mradi wa kwanza ulikua daraja la Tanzanite – Dar es Salaam, namuomba Mungu anipe uwezo niikamilishe yote,” alisema Rais, Mhe. Dkt. Samia.

Rais Samia alisema ni takribani miaka 50 toka mchakato wa Serikali kuhamishia Makao Makuu ya nchi Dodoma kutangazwa rasmi mwaka 1973, ambapo Serikali ilianza utekelezaji kwa kujenga taasisi zake mbalimbali ikiwemo Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ofisi za Bunge, Wizara ya TAMISEMI, Chuo Kikuu cha Dodoma, Hospitali ya Benjamini Mkapa na Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete pamoja na kupanua eneo ilipojengwa Ikulu hiyo kutoka heka 66 mpaka 8473.

“Katika utekelezaji wa wazo la kuhamisha Makao Makuu ya Serikali Dodoma, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli ameandika historia yake, hatutoweza kuandika historia ya shughuli hii bila ya kuwepo kwa tahariri ya mchango wake mkubwa, tuendelee kumuombea Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa Amani,” alisema Rais Samia.

Akiongelea hatua inayofuata baada ya kukamilika kwa majengo ya Ikulu hiyo Rais Samia alisema ni ujenzi wa jengo la kisasa litakaloitwa ‘Samia Complex’ ambapo litajumuisha ukumbi mkubwa wa mikutano utakaoweza kuchukua idadi ya watu 2000 – 3000, nyumba za viongozi, Zanzibar lounge, East Afrika lounge, njia ya ndege, sehemu ya historia ya viongozi pamoja na viwanja vya michezo mbalimbali.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kamba pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango kuashiria ufunguzi wa Jengo la Ikulu ya Chamwino huku viongozi mbalimbali wakishuhudia katika Sherehe zilizofanyika kwenye viwanja vya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya kumbukumbu na Marais Wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Ali Hassan Mwinyi, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Pamoja na Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein mara baada ya kuzindua Jengo la Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdalla pamoja na Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi wakati akikata Utepe kuashiria ufunguzi wa Jengo la Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdalla pamoja na Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi wakati akikata Utepe kuashiria ufunguzi wa Jengo la Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango wakati wakipiga ngoma kabla ya kuingia Rasmi katika Ofisi za Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Rasmi la Ukaguzi lililoandaliwa na Jeshi la Polisi mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023.


Viongozi wa Serikali, Viongozi wastaafu, watu mashuhuri pamoja na wananchi wengine wakiwa katika viwanja vya Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma kwa ajili ya Sherehe za ufunguzi wa Jengo la Ikulu Chamwino tarehe 20 Mei, 2023.
Taaswira ya Jengo jipya la Ikulu ya Chamwino kama linavyoonekana pichani ambalo limezinduliwa Rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 20 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikabidhi Tuzo ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa Mama Maria Nyerere wakati wa Sherehe za ufunguzi wa Jengo la Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikabidhi Tuzo ya Hayati Rais wa Awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli kwa Mama Janeth Magufuli wakati wa Sherehe za ufunguzi wa Jengo la Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa hotuba yake mara baada ya kufungua rasmi Jengo la Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Tulia Ackson pamoja na Spika wa Baraza la Waakilishi Mhe. Zubeir Ally Maulid mara baada ya kufungua Jengo la Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango pamoja na viongozi wengine wakati wakiangalia juu wakati Bendera ya Taifa, ya Rais na ile ya Afrika Mashariki ikipandishwa mara baada ya ufunguzi wa Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023. 


Post a Comment

0 Comments