Ticker

6/recent/ticker-posts

FILAMU YA KWANZA YA UBUNIFU WA KISAYANSI YAZINDULIWA

Baadhi ya Wasanii walioshiriki kwenye filami ya kisayansi EONII
Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Yahaya Mohamed akizungumza wakati wa hafla ya kutambulisha filamu mpya ya kisayansi ya "EONII " Leo Mei 29,2023 Jijini Dar es salaam

Mkurugenzi wa Studio za Power Brush Eddie Mzale akizungumza wakati wa hafla ya kutambulisha filamu mpya ya kisayansi ya "EONII " Leo Mei 29,2023 Jijini Dar es salaam

*******************

Na Magrethy Katengu

Azam Tv Kwa ushirikiano na Power Studio imezindua filamu ya kwanza yenye Ubunifu wa Kisayansi "EONII" iliyojaa simulizi za kusisimua vionjo vyenye bashasha Watanzamaji wakae mkao wa kubudika .

Akizungunza leo Jijini Dar es salaam Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Yahaya Mohamed wakati wa hafla ya kutambulisha filamu mpya ya kisayansi ya "EONII " ambapo amesema filamu hiyo inalenga kuonyesha vipaji na uwezo mkubwa ndani ya tasnia ya filamu na kutangaza kwa fahari ya wasanii kazi zao .

"Kama taasisi tukiwa na maono ya kuimarisha tasnia ya filamu ya Tanzania katoka soko la kimataifa,Azam TV na Power Brush Studio tumeshirikiana kutengeneza "EONII"kwa kutumia timu ya utayarishaji wa ndani yenye ujuzi inaonyesha simulizi wa hadithi na utaalamu wa kiufundi katoka tasnia ya filamu Tanzania na kutoa vipaji.

Afisa Mtendaji Mkuu amesema filamu hiyo imezinduliwa na itaonyeshwa katoka kumbi za filamu maarufu kama theatre kwa kiingilio nafuu sana ambapo viingilio vitatangazwa hivi karibuni katoka mikoa ikiwemo Dar es salaam ,Mwanza,Arusha,Dodoma,Tanga,kwani hiyo ni mipango ya muda mrefu hasa unapofunguliwa msimu wa utalii nao wapate fursa ya kuona ubunifu huo wa kitanzania.

"EONII" filamu imebeba hadithi ya kuvutia ugunduzi wa kisayansi katika uhitaji wa nishati ya uhakika na ombwe kubwa kukosekana kwake kunakozua taharuki katika jamii husika madoido ukisasa unaotumika kuzungumzia mkasa huu itabaki kama alama ya furaha mioyoni mwa Watanzania wengi wapenzi wa filamu"amesema Mohamedi

Kwa upande Mkurugenzi wa Studio za Power Brush Eddie Mzale aliongeza kwa kusema kuwa "timunyetu imewekeza ubunifu na maarifa yeti mioyo kuandaa "EONII " na tunajivunia sana kwa namna filamu hii ilivyotoka kuanzia ubora mpaka hadithi yenyewe hivyo tunaamini filamu hii soyo tu inavutia watazamaji ulimwengu kote lakini pia kama chachu ya ukuaji wa tasnia ya filamu ya Tanzania .

Aidha Kiu ya Serikali ya Tanzania na Wizara husika ni kuona Wasanii wanapiga hatua katika filamu zao Kimataifa Azam Media LTD na Power Brush Studio kiwahakikishia Watanzania wote kwa mchanganyiko wa vipaji vya Watanzania,Usimulizi wa hadithi za kuvutia na animations za kisiasa kabisa"EONII" bila shaka tunakwenda kuandika historia nyingine itakoyoisukuma tasnia ya filamu Tanzania katika hatua ya kimataifa

Post a Comment

0 Comments