Ticker

6/recent/ticker-posts

DC MKUDE AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI YA ZIWA VICTORIA MAGANZO


Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkud (kulia) akiweka jiwe la msingi Mradi wa upanuzi wa maji ya Ziwa Victoria Maganzo - Masagala uliopo kata ya Maganzo wilaya Kishapu Mkoani Shinyanga.


Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude ameweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa upanuzi mradi wa maji ya Ziwa Victoria Maganzo - Masagala uliopo kata ya Maganzo wilaya Kishapu Mkoani Shinyanga uliotekelezwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilayani humo.

Zoezi hilo la uwekaji wa jiwe la msingi limefanyika leo Jumatano Mei 24, 2023 katika kijiji cha Masagala kata ya Maganzo wilayani humo.

Akisoma taarifa ya ujenzi wa mradi huo Meneja wa RUWASA wilaya ya Kishapu Mhandisi Dickson Kamazima amesema ujenzi wa 
Tanki kubwa lenye ujazo wa lita laki 100,000
 umegharimu kiasi cha shilingi milioni 616 fedha kutoka serikali kuu kupitia mfuko wa taifa wa maji (NWF) na kutarajia kuhudumia vijiji viwili vilivyopo kata ya Maganzo ambapo wananchi 2500  watanufaika na mradi huo.

“Ujenzi wa tanki hili uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 616 katika mradi utakwenda kuhudumia vijiji viwili ambavyo ni kijiji cha Masagala na Maganzo.  Kukamilika kwa mradi huu itakuwa msaada mkubwa na kupunguza adha ya maji kwani utafikia jumla ya wakazi 2500 ambapo mpaka sasa ujenzi wa mradi huu umefikia asilimia 95, lengo la mradi huu ni kutoa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wa Maganzo - Masagala”, amesema Mhandisi Dickson Kamazima.

Mwenyekiti wa kijiji cha Masalaga Elias Masanja amesema uhaba wa upatikanaji wa maji kwenye kijiji cha Masagala iliwalazimu akina mama kuamka saa 10 alfajiri kwenda kutafuta maji lakini kwa sasa kukamilika kwa upanuzi wa maji ya Ziwa Victoria kwenye eneo hilo kutapunguza adha ya maji kwa wananchi.

“Uhitaji wa maji kwenye kijiji chetu cha Masagala ulikuwa ni mkubwa kutokana na uhaba wa visima vya maji na kupelekea akina mama kuamka saa 10 usiku kwenda kutafuta maji ambapo ilihatarisha maisha yao lakini kwa sasa watalala usingizi mnono, tunawapongeza na kuwashukuru RUWASA kwa kusogeza huduma hii ya maji, niwaombe maji haya yafike na vitongoji vingine”, amesema Elias Masanja.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Maganzo Lwinzi Kidiga ameipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ujenzi wa miradi kwenye maeneo mbalimbali hususa ni miradi ya maji inayoendelea kutekelezwa.

Naye Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude mara baada ya kufungua mradi huo amewapongeza Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini ngazi ya mkoa na wilaya kwa utekelezaji wa miradi ya maji kikamilifu na kuwataka wananchi kuitunza miundombinu hiyo ili idumu kwa muda mrefu.

“Utunzaji wa miradi hii ni muhimu hivyo tuhakikishe tunatunza mazingira ya eneo hili la mradi, matanki na mabomba yake, lakini pia mradi huu utakua unajiendesha kupitia fedha mtakazo lipa, hivyo nitoe wito kwa wananchi kusogeza maji kwenye kaya zanu, hakuna haja ya kwenda kuchota maji kwenye magati”, amesema Joseph Mkude.

Wakati huo huo Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini RUWASA wilayani Kishapu wameendesha mkutano mkuu wa mwaka wa wadau wa maji wenye lengo la kujadili na kubadilishana uzoefu kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu maji na usafi wa mazingira.
Meneja wa RUWASA wilaya ya kishapu Mhandisi Dickson akisoma taarifa ya ujenzi wa mradi huo.
Meneja RUWASA Mkoa wa Shinyanga Julieth Payovela akizungumza
Mwenyekiti wa kijiji cha Masalaga Elias Masanja  akizungumza baada ya zoezi la uwekaji wa jiwe la msingi kwenye mradi huo.
Diwani wa kata ya Maganzo Lwinzi Kidiga  akizungumza.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude  akizungumza mara baada ya kuweka jiwe la msingi.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkud (kulia) akiweka jiwe la msingi Mradi wa upanuzi wa maji ya Ziwa Victoria Maganzo - Masagala uliopo kata ya Maganzo wilaya Kishapu Mkoani Shinyanga.
Mradi wa upanuzi wa maji ya Ziwa Victoria Maganzo - Masagala uliopo kata ya Maganzo wilaya Kishapu Mkoani Shinyanga.
Wadau wa maji wilayani Kishapu wakati wa mkutano mkuu na wadau wa maji wilayani Kishapu.
Meneja wa RUWASA wilaya ya kishapu Mhandisi Dickson akizungumza wakati wa mkutano na wadau wa maji wilayani Kishapu.
Meneja RUWASA Mkoa wa Shinyanga Julieth Payovela  wakati wa mkutano mkuu na wadau wa maji wilayani Kishapu.
Wadau wa maji wilayani Kishapu wakati wa mkutano mkuu na wadau wa maji wilayani Kishapu.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza wakati wa mkutano na wadau wa maji wilayani Kishapu.
Meneja RUWASA Mkoa wa Shinyanga Julieth Payovela  kushoto akiwa na Meneja RUWASA wilaya ya Kishapu  Dickson Kamazima wakati wa mkutano na wadau wa maji wilayani Kishapu.

Post a Comment

0 Comments