Ticker

6/recent/ticker-posts

ATCL YASHEHEREKEA UREJESHWAJI WA SAFARI ZAKE DAR-GUANGZHOU





Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imesheherekea urejeshwaji wa safari zake za Dar es Salaam kwenda Guangzhou kwa kusafirisha abiria 78 wakiwemo ujumbe wa makampuni 25 yanayoongoza kwa watalii nchini China. 

Ujumbe huo umeambatana na vyombo 6 vya habari mashuhuri kutoka nchini humo na umewasili na Air Tanzania kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Amani Abeid Karume, Zanzibar ukitokea Guangzhou, China.


Akizungumza wakati wa mapokezi, Hafsa Mbamba Katibu Mtendaji Kamisheni ya Utalii Zanzibar amesema Ujumbe huo muhimu kutoka Sekta ya Utalii nchini China pamoja na Wanahabari wa Vyombo vikubwa nchini huko
utapata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya vivutio vilivyopo Zanzibar, Arusha na Dar es Salaam. 


Naye Edward Nkwabi Meneja Biashara ATCL amesema Kampuni ya Ndege Tanzania imerejesha safari zake za Dar kwenda Guangzhou ambapo watatumia ndege ya kisasa Boieng 787-8 yenye uwezo wa kubeba takribani abiria 262 kwa na mizigo tani 20.


Amefafanua kuwa kwa sasa ndege hiyo inafanya safari zake za Guangzhou China, mara tatu kwa wiki ambapo ni kila Jumanne, Alhamisi na Jumamosi.


Ziara hiyo imeandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini China kwa kushirikiana na Kampuni ya Ndege Tanzania, Bodi ya Utalii Tanzania, Kamisheni ya Utalii Zanzibar pamoja na Benki ya NMB.

Post a Comment

0 Comments