Ticker

6/recent/ticker-posts

WORLD VISION TANZANIA YAZINDUA MRADI WA NOURISH KISHAPU SHINYANGA

Mkurugenzi wa Miradi wa World Vision Tanzania Dkt. Gideon Cohen akizungumza wakati Shirika la World Vision Tanzania likizindua Mradi wa NOURISH utakaotekelezwa katika kata ya Ngofila na Lagana wilaya ya Kishapu
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi  akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme wakati Shirika la World Vision Tanzania likizindua Mradi wa NOURISH utakaotekelezwa katika kata ya Ngofila na Lagana wilaya ya Kishapu

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Shirika la World Vision Tanzania limezindua Mradi wa NOURISH wenye lengo la kupunguza umaskini na njaa katika kaya na jamii zilizo katika mazingira hatarishi utakaotekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano katika kata za Ngofila na Lagana Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoa wa Shinyanga.

Mradi huo umezinduliwa leo Jumatano Aprili 12, 2023 na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme katika ukumbi wa Vigirmark Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali.

Akizungumza wakati wa kikao cha Kutambulisha Mradi wa NOURISH kwa viongozi na maafisa wa serikali,  Mhe. Samizi amelipongeza Shirika la World Vision kwa kupeleka mradi huo katika wilaya ya Kishapu akibainisha kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Shirika la World Vision Tanzania na wadau mbalimbali kuhakikisha mradi huo unakuwa na tija kwa wananchi.

“Utambulisho wa Mradi huu ni takwa la Kisheria kwa mujibu wa Sheria Na. 24 ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Mwaka 2002 pamoja na Mwongozo wa uratibu wa mashirika yasiyo ya kiserikali ya mwaka 2020. Utambulisho wa mradi huu unatoa fursa ya uwazi wa uwajibikaji lakini pia kujadiliana kwa pamoja kuhusu muundo wa mradi (Project Design) na kufanya marekebisho ya afua ambazo zinaweza kuleta mkanganyiko dhidi ya kanuni, sheria, taratibu na maadili ya nchi zetu”,ameeleza Mhe. Samizi.
“Nipongeze Shirika la World Vision Tanzania kwa kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali inayoendana na vipaumbele vya serikali hususani ujenzi wa miundombinu ya afya, elimu, maji, lishe na afua za uimarishaji wa kaya kwa wananchi wenye hali duni ya kipato”,amesema.

“Tunawashukuru sana World Vision Tanzania kwa mradi huu, matarajio yetu ni kuona mradi unaleta tija katika jamii. Mmekuwa wadau wazuri katika utekelezaji wa miradi inayogusa moja kwa moja wanajamii hasa wanaoishi katika mazingira magumu na kuwezesha ustawi wa mtoto katika mkoa wa Shinyanga”,amesema Samizi.

Aidha ametumia fursa hiyo kuyakumbusha mashirika na taasisi mbalimbali zinazotekeleza miradi katika jamii kuhakikisha wanatekeleza kwa kuzingatia mila na desturi ili kulinda maadili na utamaduni wa Mtanzania.
Mkurugenzi wa Miradi wa World Vision Tanzania Dkt. Gideon Cohen

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Miradi wa World Vision Tanzania Dkt. Gideon Cohen amesema ili kutekeleza mradi wa NOURISH kikamilifu ni lazima wadau wote washirikiane.

“Mradi huu wa NOURISH siyo mradi wa World Vision pekee bali ni mradi wa Watanzania wote, naomba tushirikiane sote ili kupata matokeo chanya”,amesema Dkt. Cohen.

Meneja wa World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa, Jackline Kaihira amesema mradi wa NOURISH unagusa maeneo mbalimbali yakiwemo ya Lishe na afya na usawa wa kijinsia na uchumi hivyo kuwaomba wadau wote kushirikiana ili kutimiza malengo ya mradi.
Meneja wa World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa, Jackline Kaihira.

Amesema Mradi huo utafanya kazi katika Nyanja za afya, lishe, kilimo, kuimarisha uchumi wa kaya na masuala ya kijinsia na kwamba wameamua kukutana na wadau ili wajue shughuli za mradi kiundani,kupitia mpango kazi wa mwaka wa kwanza na kuhuisha mipango ya serikali na ile ya mradi ili kuweza kushirikiana kwa karibu katika utekelezaji.

Mratibu wa Mradi wa NOURISH Irene Abusheikh amesema lengo la mradi wa NOURISH (Nature – Based Opportunities Underpinning Resilient and Sustainable Households) ni kupunguza umaskini na njaa katika kaya na jamii zilizo katika mazingira hatarishi ambapo walengwa wakuu ni wanawake na watoto waliopo kwenye jamii.

Amesema mradi huo utatekelezwa na Shirika la World Vision Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Kivulini na serikali.

Afisa Mwandamizi Kivulini, Eunice Mayengela amesema Kivulini inashiriki katika mradi wa NOURISH kwa kuwezesha wanawake kijamii na kiutamaduni hususani katika kuwajengea uwezo wa kushiriki katika nafasi mbalimbali za maamuzi kuanzia ngazi ya familia na jamii.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Emmanuel Johnson amesema wamepokea vizuri mradi huo na kuongeza kuwa utaongeza chachu katika masuala ya afya, lishe na kukuza uchumi wa wananchi.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi  akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme wakati Shirika la World Vision Tanzania likizindua Mradi wa NOURISH utakaotekelezwa katika kata ya Ngofila na Lagana wilaya ya Kishapu
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi  akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme wakati Shirika la World Vision Tanzania likizindua Mradi wa NOURISH utakaotekelezwa katika kata ya Ngofila na Lagana wilaya ya Kishapu
Mkurugenzi wa Miradi wa World Vision Tanzania Dkt. Gideon Cohen akizungumza wakati Shirika la World Vision Tanzania likizindua Mradi wa NOURISH utakaotekelezwa katika kata ya Ngofila na Lagana wilaya ya Kishapu
Mkurugenzi wa Miradi wa World Vision Tanzania Dkt. Gideon Cohen akizungumza wakati Shirika la World Vision Tanzania likizindua Mradi wa NOURISH utakaotekelezwa katika kata ya Ngofila na Lagana wilaya ya Kishapu
Mkurugenzi wa Miradi wa World Vision Tanzania Dkt. Gideon Cohen akizungumza wakati Shirika la World Vision Tanzania likizindua Mradi wa NOURISH utakaotekelezwa katika kata ya Ngofila na Lagana wilaya ya Kishapu
Meneja wa World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa, Jackline Kaihira akizungumza wakati Shirika la World Vision Tanzania likizindua Mradi wa NOURISH utakaotekelezwa katika kata ya Ngofila na Lagana wilaya ya Kishapu

Mratibu wa Mradi wa NOURISH Irene Abusheikh akielezea kuhusu Mradi wa NOURISH utakaotekelezwa katika kata ya Ngofila na Lagana wilaya ya Kishapu

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Emmanuel Johnson akizungumza wakati Shirika la World Vision Tanzania likizindua Mradi wa NOURISH
 Afisa Mwandamizi Kivulini, Eunice Mayengela akielezea namna Kivulini itakavyoshiriki katika  utekelezaji wa mradi wa NOURISH wilayani Kishapu

Wadau wakiwa ukumbini wakati Shirika la World Vision Tanzania likizindua Mradi wa NOURISH

Picha ya kumbukumbu wakati Shirika la World Vision Tanzania likizindua Mradi wa NOURISH

Picha ya kumbukumbu wakati Shirika la World Vision Tanzania likizindua Mradi wa NOURISH.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Post a Comment

0 Comments