Mkurugenzi wa kampuni ya Bison Engineering Co Ltd inayojenga miradi wa maji mkoani Mtwara Abiud Kamando wa kwanza kushoto,akizungumza na baadhi ya wafanyakazi Wakala wa maji safi na usafi wa mazingira(Ruwasa)mkoani Mtwara,wa tatu kulia Mbunge wa Jimbo la Ndanda Cecil Mwambe.
Baadhi ya watumishi wa wakala wa maji safi na usafi wa mazingira wilaya ya Newala na mkoa wa Mtwara wakiwa katika picha ya pamoja na Mkandarasi wa kampuni ya ULM Investment Mwanahamisi Ngalemwa wa tatu kulia aliyejenga mradi wa maji Mandala wilayani Newala.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2023 Abdallah Shaib Kaim,akinywa maji baada ya kuzindua rasmi mradi wa maji Mandala wilayani Newala.
Meneja wa Ruwasa wilayani Newala Mhandisi Sadik Nsajigwa kushoto,akimuangalia kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdala Shaib Kaim alipokuwa akifungua koki katika moja ya vituo vya kuchotea maji katika kijiji cha Mandala wilayani humo.
*******************
Na Muhidin Amri,
Mtwara
WAKANDARASI wanaotekeleza miradi ya maji mkoani Mtwara,wameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwaamini na kuwapatia kazi nyingi za miradi ya maji katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya mkoa huo.
Wamesema,katika kipindi cha miaka miwili cha uongozi wa Rais Dkt Samia ndiyo chenye mafanikio makubwa zaidi kwa sababu wana uhakika wa kupata kazi nyingi za miradi na malipo yao kufanyika kwa wakati muafaka.
Abiud Kamando mkurugenzi wa kampuni ya Bison Engineering Co Ltd amesema,mageuzi yaliyofanywa na serikali kwenye sekta ya maji yamewasaidia sana wakandarasi wazawa kuwajengea uwezo na kuwa na uthubutu katika kutekeleza miradi midogo na mikubwa.
Kamando amesema,sehemu kubwa ya miradi hiyo imepunguza changamoto kubwa ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi hasa wanaoishi maeneo ya vijijini.
“tunaipongeza sana serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wetu mpendwa Dkt Samia Suluhu Hassan kutupa fursa hii ya kuwa sehemu ya watekelezaji wa kauli mbiu ya Mheshimiwa Rais Dkt Samia ya kumtua mama ndoo kichwani katika mkoa wa Mtwara”alisema.
Amesema,hapo awali changamoto kubwa ilikuwa kupata kazi na kuchelewa kwa malipo hata baada ya kukamilisha kazi,jambo lililo sababisha baadhi ya miradi kutokamilika kwa wakati.
Kamando ameiomba serikali, kuendelea kuwaamini wakandarasi wadogo na wazawa kwa kuwapa kazi nyingi ili kuwajengea uwezo wa kifedha na uzoefu utakao wasaidia kutekeleza miradi ya maji kwa ubora.
Kamando kupitia kampuni yake amehaidi kuwa mwaminifu,kutumia weledi na kasi kubwa katika kutekeleza miradi ili kuunga mkono malengo ya serikali kumaliza shida ya huduma ya maji chini ya kauli mbiu ya Rais Samia ya kumtua mama ndoo kichwani.
Ametoa wito kwa wakandarasi wenzake kuwa wazalendo kwa nchi yao,waadilifu na kutanguliza maslahi ya nchi mbele kwa kutekeleza miradi kwa wakati na yenye viwango ili kuisaidia serikali kutimiza adhima yake ya kumaliza kero ya huduma ya maji kwa Watanzania.
Mkandarasi wa kampuni ya ULM Investment Mwanahamisi Ngalemwa,ameushukuru wakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa) kuwapa kazi za miradi ya maji wakandarasi wanawake na kueleza kuwa,hatua hiyo itawawezesha kupata uzoefu na kupata mitaji.
Ngalemwa ambaye ni mwanamke pekee anayefanya kazi za ukandarasi mkoani Mtwara,amemshukuru meneja wa Ruwasa katika mkoa huo Mhandisi Primy Damas na timu yake kwa kuwajali na kuwathamini wakandarasi wadogo.
Amesema,hatua hiyo imewafanya kuamini katika taasisi za fedha kwa kupata mikopo ambayo imewasaidia sana kutekeleza majukumu yao bila kutegemea malipo ya awali kutoka serikalini.
Ngalemwa,amempongeza na kumshukuru Meneja wa Ruwasa mkoani Mtwata Mhandisi Primy Damas kwa kuwajali wakandarasi na kuhakikisha wanalipwa fedha zao kwa wakati na kuwataka wakuu wa idara na taasisi nyingine za serikali kuiga mfano wa Damas katika kutekeleza na kusimamia majukumu yake.
0 Comments