Ticker

6/recent/ticker-posts

TCRA YATOA MWONGOZO WA KUSAFIRISHA VIFURUSHI NA VIPETO

 


Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Katika kukabiliana na vitendo vya udanganyifu, utapeli na upotevu wa mizigo wakati wa usafirishaji wa vifurushi na nyaraka mbalimbali (Vipeto), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezitaka Kampuni zinazotoa huduma hiyo kutimiza matakwa ya kisheria kwa kukata leseni ya usafirishaji vifurushi na vipeto kutoka TCRA

Kipeto ni mzigo mdogo wa angalau kilo moja au chini ya hapo na kifurushi ni kikubwa kuliko kipeto. Kifurushi huwa na uzito wa hadi angalau kilo 20 au 30.


Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi leo Aprili 20,2023 Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo amesema kuwa na leseni ya kusafirisha vifurushi na vipeto ni muhimu kwa sababu inaruhusu mtu au kampuni kufanya biashara ya usafirishaji wa bidhaa hizo za kiposta kwa njia halali na yenye kufuata Sheria na Kanuni za usafirishaji.


Amesema Leseni hiyo inahakikisha kuwa mtoaji huduma ya usafirishaji amefuata taratibu zote muhimu kwa ajili ya usalama wa bidhaa na kuepuka adhabu ya kisheria.


Amezitaja baadhi ya sababu za umuhimu wa kuwa na leseni ya kusafirisha vifurushi na vipeto ni kwamba Leseni inahakikisha Mtoa Huduma/ kampuni au mtu binafsi anayefanya biashara ya usafirishaji wa bidhaa za kipeto vikiwemo vipeto na vifurushi amefuata sheria na kanuni za usafirishaji. 

"Hii ni muhimu kwa sababu Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (2010) Kifungu cha Sita kinaelekeza Dhahiri kwamba Mtu Yeyote au Kampuni inayotaka kutoa Huduma za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta sharti aombe na kupatiwa Leseni inayotolewa na TCRA",ameeleza.
Sababu nyingine ni kwamba Leseni ya usafirishaji vipeto na vifurushi inaweza kuongeza uaminifu wa wateja kwa kampuni au mtu binafsi anayetoa huduma za usafirishaji wa bidhaa. Hii ni kwa sababu leseni inathibitisha kuwa mtoaji huduma anafuata taratibu na kanuni za usalama za kusafirisha vifurushi na vipeto.


Hali kadhalika Leseni inaweza kusaidia kampuni au mtu binafsi anayefanya biashara ya usafirishaji wa bidhaa kuwa na uwezo wa kudhibiti hatari za usafirishaji wa bidhaa. Leseni inaweza kusaidia kampuni au mtu binafsi kuelewa sheria za usafirishaji wa bidhaa na kuzuia uwezekano wa kupoteza au kuharibiwa kwa bidhaa au kusafirisha bidhaa zilizozuiwa kwa mujibu wa sheria.


“Kwa hiyo, kuwa na leseni ya kusafirisha vifurushi na vipeto ni muhimu sana kwa sababu inahakikisha kuwa biashara ya usafirishaji wa bidhaa inafuata sheria na kanuni za usalama na kuongeza uaminifu wa wateja”,ameongeza Mhandisi Mihayo.


Mhandisi Mihayo amesema Leseni ya usafirishaji wa vifurushi na vipeto (Courier Service License) hutolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa mujibu wa Sheria ya Mawasiliano ya Elektroniki na Posta ya mwaka 2010.


“TCRA imerahisisha sana upataji wa Leseni za Mawasiliano. Kwa sasa unahitaji kujisajili kwenye tovuti ya Tanzanite ambayo inapatikana kwa kiunganishi cha www.tanzanite.tcra.go.tz . Ukiingia hapo jisajili kisha jaza fomu za maombi ya leseni kwa kuzingatia aina ya leseni unayotaka kuomba”,amesema Mhandisi Mihayo.


Mhandisi Mihayo amesema TCRA imezindua kampeni ya elimu ya umma ili kuwaelimisha watumiaji wa huduma za usafirishaji vipeto na vifurushi kuwa na ufahamu wa kutumia watoa huduma waliosajiliwa/wenye leseni za kutoa huduma husika ambapo kampeni hii inalenga kuwakumbusha watoa huduma kusajili biashara/huduma zao na kuzingatia sheria na kanuni zinazosimamia sekta hiyo.


“Kwa kawaida, watumiaji wa huduma hizi baadhi yao hawajui nani ni mtoa huduma aliyesajiliwa, hivyo kampeni hii inawaelimisha wananchi kwamba mtoa huduma aliyesajiliwa Taarifa zake zinapatikana kwenye dawati la duka lake (kwa kuonesha leseni-inayopaswa kuwekwa mahali panapoonekana aghalabu ukutani). Pia mtoa huduma aliyesajiliwa Taarifa zao zinapatikana kwenye tovuti ya TCRA www.tcra.go.tz ambako kuna orodha kamili ya wenye leseni”,ameeleza Mhandisi Mihayo.

“Tunaposema Tuma Chap kwa Usalam tunamaanisha Mwananchi azingatie kutuma kipeto/kifurushi chake kwa mtoa huduma aliyesajiliwa, kwani kufanya hivyo kunaiwezesha TCRA kufuatilia Haki na Wajibu kwa pande zote mbili mfano mtoa huduma na anayehudumiwa",amesema.
Amesema kuzinduliwa kampeni Tuma Chap kwa Usalama ni sehemu ya majukumu ya TCRA katika kuendeleza kuongeza uelewa wa umma kuhusu umuhimu wa kutumia watoa huduma waliosajiliwa wa kubeba Vipeto na Vifurushi na kuwakumbusha watoa huduma kuzingatia sheria na kanuni za sekta hiyo kwa lengo la kuboresha usalama wa Vipeto na Vifurushi inayosafirishwa na kuimarisha biashara katika sekta ya kubeba Vipeto na Vifurushi nchini Tanzania.


MWANANCHI AZINGATIE NINI KABLA YA KUTUMA KIPETO/KIFURUSHI

“Kabla ya kumkabidhi msafirishaji Kifurushi au Kipeto, mwananchi anatakiwa kuzingatia kama Mtoa Huduma ana na Leseni inayomruhusu kusafirisha vipeto na vifurushi. Pia mwananchi ahakikishe anapatiwa Risiti ya Utumaji mzigo, ahakikishe anamjulisha msafirishaji bidhaa inayosafirishwa na ikaguliwe,ahakikishe anapatiwa namba ya kufuatilia mzigo (tracking number) na ahakikishe kipeto au kifurushi chake kimefungwa vizuri, na kama ni mali ya kuharibika kirahisi kv chupa nk aweke bayana kwa kuweka maandishi yanayotahadharisha wabebaji”,ameeleza Mhandisi Mihayo.

“Mwananchi ananufaika kwa kutumia msafirishaji wa vifurushi na vipeto mwenye Leseni ya TCRA kwa njia kadhaa kama vile Usalama wa vifurushi na vipeto ambapo Msafirishaji mwenye leseni ya TCRA anawajibika kuhakikisha kuwa vifurushi na vipeto vyote vinavyosafirishwa vinawasili salama na katika hali nzuri lakini pia Msafirishaji mwenye leseni ya TCRA anawajibika kutoa huduma ya haraka na kwa wakati kwa wateja wake, hivyo kurahisisha shughuli za biashara kwa wateja wake”,amesema.


“Pia faida nyingine ni kwamba Msafirishaji mwenye leseni ya TCRA hutoa huduma ya kuchukua na kuleta vifurushi na vipeto moja kwa moja kwa mlango wa mteja wake, hivyo kuwapa wateja wake urahisi wa kusafirisha bidhaa. Hali kadhalika Msafirishaji mwenye leseni ya TCRA hutoa huduma za usafirishaji kwa bei nafuu na kwa ushindani mkubwa katika soko kwa kuwa TCRA inasimamia ushindani wa kibishara wenye kuzingatia haki kwa mtumiaji huduma”,ameongeza Mhandisi Mihayo.


Amefafanua kuwa Msafirishaji mwenye leseni ya TCRA hutoa huduma ya kufuatilia vifurushi na vipeto kwa njia ya kielektroniki, hivyo kutoa uhakika kwa wateja wake kuwa vifurushi na vipeto vyao vinawasili salama na kwa wakati uliopangwa.

“Kwa hiyo, kutumia msafirishaji wa vifurushi na vipeto mwenye Leseni ya TCRA kunampa mteja uhakika wa huduma bora, salama, haraka na kwa gharama nafuu, hivyo kumwezesha kufanya biashara yake kwa ufanisi zaidi”,amesema.


“Kabla ya kumkabidhi msafirishaji Kifurushi au Kipeto, mwananchi anatakiwa kuzingatia kama Mtoa Huduma ana na Leseni inayomruhusu kusafirisha vipeto na vifurushi. Pia mwananchi ahakikishe anapatiwa Risiti ya Utumaji mzigo, ahakikishe anamjulisha msafirishaji bidhaa inayosafirishwa na ikaguliwe,ahakikishe anapatiwa namba ya kufuatilia mzigo (tracking number) na ahakikishe kipeto au kifurushi chake kimefungwa vizuri, na kama ni mali ya kuharibika kirahisi kv chupa nk aweke bayana kwa kuweka maandishi yanayotahadharisha wabebaji”,ameeleza Mhandisi Mihayo.
“Mwananchi ananufaika kwa kutumia msafirishaji wa vifurushi na vipeto mwenye Leseni ya TCRA kwa njia kadhaa kama vile Usalama wa vifurushi na vipeto ambapo Msafirishaji mwenye leseni ya TCRA anawajibika kuhakikisha kuwa vifurushi na vipeto vyote vinavyosafirishwa vinawasili salama na katika hali nzuri lakini pia Msafirishaji mwenye leseni ya TCRA anawajibika kutoa huduma ya haraka na kwa wakati kwa wateja wake, hivyo kurahisisha shughuli za biashara kwa wateja wake”,ameeleza.


“Pia faida nyingine ni kwamba Msafirishaji mwenye leseni ya TCRA hutoa huduma ya kuchukua na kuleta vifurushi na vipeto moja kwa moja kwa mlango wa mteja wake, hivyo kuwapa wateja wake urahisi wa kusafirisha bidhaa. Hali kadhalika Msafirishaji mwenye leseni ya TCRA hutoa huduma za usafirishaji kwa bei nafuu na kwa ushindani mkubwa katika soko kwa kuwa TCRA inasimamia ushindani wa kibishara wenye kuzingatia haki kwa mtumiaji huduma”,ameongeza.


Amefafanua kuwa Msafirishaji mwenye leseni ya TCRA hutoa huduma ya kufuatilia vifurushi na vipeto kwa njia ya kielektroniki, hivyo kutoa uhakika kwa wateja wake kuwa vifurushi na vipeto vyao vinawasili salama na kwa wakati uliopangwa.

“Kwa hiyo, kutumia msafirishaji wa vifurushi na vipeto mwenye Leseni ya TCRA kunampa mteja uhakika wa huduma bora, salama, haraka na kwa gharama nafuu, hivyo kumwezesha kufanya biashara yake kwa ufanisi zaidi”,amesema.

“Majukumu ya TCRA katika usimamizi wa usafirishaji wa vifurushi na vipeto ni pamoja na kusimamia watoa huduma za usafirishaji vifurushi na vipeto na huduma za Posta. TCRA ina jukumu la kusimamia na kudhibiti huduma zote za mawasiliano nchini Tanzania, zikiwemo huduma za usafirishaji vifurushi na vipeto kama sehemu ya huduma za posta”,ameeleza Mhandisi Mihayo.


Majukumu mengine ya TCRA ni kutoa leseni kwa wanaohitaji kutoa huduma za Posta ambazo zinahusisha usafirishaji vifurushi na vipeto ambapo TCRA inatoa leseni kwa watoa huduma za mawasiliano kama vile kampuni za simu za mkononi, kampuni za intaneti, na vituo vya redio na televisheni pamoja na Posta. Huduma za usafirishaji vipeto na vifurushi katika mukhtadha huu zimo katika kundi la huduma za Posta.


Pia TCRA ina jukumu la kulinda haki za watumiaji wa huduma za mawasiliano ambapo TCRA inalinda haki za watumiaji wa huduma za mawasiliano kwa kuhakikisha kwamba watoa huduma wanafuata kanuni na taratibu zilizowekwa na TCRA na kutoa huduma bora kwa watumiaji.

“Hapa ndipo unakuja Umuhimu wa Mwananchi kuhakikisha anatuma kipeto chake kwa mtoa huduma aliyesajiliwa ili iwe rahisi zaidi kwa TCRA kulinda haki za Mwananchi kama mtumiaji wa huduma.

“Pia TCRA tuna jukumu la kusimamia usalama wa huduma zitolewazo TCRA inasimamia usalama wa huduma za usafirishaji vipeto na vifurushi kwa kuhakikisha kwamba mtoa huduma anazingatia sheria na Masharti ya Leseni wakati wote anapotoa huduma ya kusafirisha vipeto na vifurushi. Kwa hiyo, TCRA ina jukumu la kutoa leseni kwa watoa huduma za posta nchini Tanzania, kusimamia ubora wa huduma za posta, kushughulikia malalamiko ya watumiaji, na kuhakikisha usalama wa mawasiliano yanayohusisha usafirishaji wa vifurushi na vipeto kama bidhaa za kiposta", amesema.


TCRA pia inaweza kushirikiana na wadau wengine, kama vile Shirika la Posta Tanzania (TPC), katika kusimamia na kuboresha huduma za posta nchini Tanzania, ikiwa ni pamoja na usafirishaji wa vifurushi na vipeto.

Linda thamani ya mzigo wako; tumia Mtoa Huduma mwenye Leseni halali kutoka TCRA. Kwa maelezo zaidi, wasiliana na TCRA kupitia 0800008272 Bure.

TAZAMA ZAIDI HAPA


Post a Comment

0 Comments