Ticker

6/recent/ticker-posts

SIMAI AHIDI KUTOA MILIONI 3 KWA KILA GOLI LA SIMBA SC NCHINI MOROCCO


Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said (mwenye kofia nyeupe) Akizungumza

**********************

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mh. Simai Mohammed Said amekipongeza kikosi cha klabu ya Simba kwa ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco huku akiahidi kutoa milioni 3 kwa kila goli la ushindi kwenye mchezo wa marudiano nchini Morocco.

Mh. Simai amesema hayo akiwa ameshiriki katika mechi hiyo ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika (CAF CL) akishuhudia Jean Othos Baleke ikiipatia Simba goli pekee la ushindi mpaka dakika 90 za mchezo huo uliochezwa uwanja mkubwa wa Taifa wa Benjamin William Mkapa,Temeke Dar es Salaam.

Ambapo Mh.Simai amesema Wizara yake katika kumuunga mkono Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe Dk. Samia Suluhu Hassan katika kushajihisha Utalii kupitia michezo, na yeye amewaahidi Wekundu hao Klabu ya Simba kuwapa Milioni tatu kwa kila goli katika mchezo wa pili wa marudiano huko Morocco.

"Kwa kweli Simba wameonesha kuwa Mabalozi wazuri katika kuitangaza Tanzania na Utalii wetu,

Juhudi zao ni vyema Watanzania kuziunga mkono, nitatoa motisha kwa kila goli," amesema Simai wakati wa tukio la utowaji wa pesa Milioni 5 za Rais Samia ambazo anatoa kwa kila goli.

Post a Comment

0 Comments