Ticker

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YAWATOA HOFU WATANZANIA KUHUSU UGONJWA WA MARBURG

Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 4,2023 wakati akitoa taarifa kuhusu mwenendo wa ugonjwa wa Marburg uliogundulika Bukoba mkoani Kagera hivi karibuni.
Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 4,2023 kuhusu mwenendo wa ugonjwa wa Marburg uliogundulika Bukoba mkoani Kagera hivi karibuni.
Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 4,2023 wakati akitoa taarifa kuhusu mwenendo wa ugonjwa wa Marburg uliogundulika Bukoba mkoani Kagera hivi karibuni.

**********************

NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI BLOG

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imewahakikishia watanzania na jamii ya Kimataifa kuwa Tanzania ni salama dhidi ya ugonjwa wa Marburg uliogundulika Bukoba mkoani Kagera hivi karibuni.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 4,2023 Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema hadi kufikia leo jumla ya visa nane na kati ya yao watano wamefariki na mmoja amekiwa tayari ameruhusiwa na wawili wkiendelea na matibabu.

"Leo tumemruhusu mgonjwa mmoja mwanaume mwenye umri wa miaka 26 akiwa na afya njema,Ni matumaini yangu kuwa jamii itapokea vyema na kushirikiana nae katika shughuli zake za kila siku". Amesema Mhe. Ummy.

Aidha amesema jumla ya watu 212 waliotangamana na wagonjwa wamebainishwa kati ya hawa watu 35 wamemaliza siku 21 za utangulizi bila kuonesha dalili zozote za ugonjwa huu na hivyo wamewaruhusu kutoka katika karantini na kurejea kwenye familia na shughuli zao.

Pamoja na hayo Waziri amesema Serikali inahimiza wananchi wote hasa wa Mkoa wa Kagera kuendelea kuchukua tahadhari ya kudhibiti na kuzuia maambukizi mapya katika jamii.

"Tuepuke kumgusa mgonjwa au majimaji ya mwili wake ikiwemo mate, machozi, damu, mkojo, kinyesi pamoja na matandiko na nguo za mgonjwa bila kinga". Amesema

Waziri ameongeza kuwa kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), hata pale mgonjwa wa mwisho kupona atakaporugusiwa hawana budi kuendelea kuchukua tahadhari hadi watakapojiridhisha kwamba ugonjwa umeisha.

Post a Comment

0 Comments