Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis amesema suala la utatuzi wa changamoto za Muungano halijakwama wala halijasuasua.
Amesema hayo jana wakati akijibu swali la Mbunge wa Same Magharibi Mhe. Dkt. David Mathayo David aliyetaka kujua ni changamoto zipi za Muungano zimetatuliwa na zipi zimebaki.
Mhe. Khamis amesema kuwa hadi sasa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) zimejadili na kuzipatia ufumbuzi jumla ya changamoto 22 zikiwemo Gharama za Kushusha Mizigo Bandari ya Dar es Salaam kwa Mizigo inayotoka Zanzibar na Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia.
Akiendelea kujibu swali hilo amesema kuwa Hoja zilizobakia kutatuliwa ni nne ambazo ni Mapendekezo ya Tume ya Pamoja ya Fedha, Usajili wa Vyombo vya Moto, Uingizaji wa Sukari katika Soko la Tanzania Bara na Mgawanyo wa Mapato Yatokanayo na Hisa za SMZ zilizokuwa katika Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki na Faida ya Benki Kuu.
Hata hivyo, amesema Hoja nne zinazoendelea kutafutiwa ufumbuzi ni pamoja na Mapendekezo ya Tume ya Pamoja ya Fedha, Usajili wa Vyombo vya Moto,
Uingizaji wa Sukari katika Soko la Tanzania Bara na Mgawanyo wa Mapato Yatokanayo na Hisa za SMZ zilizokuwa katika Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki na Faida ya Benki Kuu.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akijibu maswali bungeni wakati wa kikao cha Bunge kabla ya kuwasilishwa kwa Hotuba ya Mapitio ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa mwaka 2022/23 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2023/24.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa na Naibu Waziri wake Mhe. Khamis Hamza Khamis wakati wa kikao cha kuwasilisha bungeni Hotuba ya Mapitio ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa mwaka 2022/23 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2023/24.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiteta jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama wakati wa kikao cha Bunge cha kuwasilisha bungeni Hotuba ya Mapitio ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa mwaka 2021/22 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2022/23 ya Ofisi ya Makamu wa Rais.
0 Comments