Na Shemsa Mussa KAGERA
Mkuu wa Mkoa Kagera Mhe Albert John Chalamila awesasisitiza wazazi na walezi wenye watoto katika shule zenye ghalama kuwa mabalozi na kutoa elimu kwa wazazi wanaokataa kutoa michango ya uji na chakula kwenye shule za kawaida (bure) .
Ameyasema hayo katika siku ya mahafali ya kidato cha sita katika shule za Kemebos na Kaizirege zilizopo katika kijiji cha ijuganyondo kata ijuganyondo manispaa ya Bukoba Mkoa kagera yaliyofanyika Aplr 29, 2023.
"Ninyi wazazi mnalipa ghalama kubwa hapa Kaizirege na Kemebos na pengine kwa kujinyima ili mtoto apate elimu bora , ila wapo wazazi wamewapeleka watoto kwenye shule za kawaida na pengine bure kabisa ila mzazi ukimwambia mchango wa uji na chakula kwa mtoto wake maelezo yanakuwa mengi,sasa nyie wazazi wenye watoto hapa nendeni mkawe mabalozi wazuri huko .amesema Chalamila"
Pia ameendelea kuwasisitiza wananchi kuendelea kuitizama shule hiyo kama kioo cha shule za Mkoa Kagera na kuendelea kutoa ushirikiano bila choyo na fitina ili mkoa ukue katika sekta ya elimu kupitia shule hiyo na nyingine.
" Mwenye shule ambaye ni Bw Yusto amejitafuta miaka mingi akiwa mvuvi na kuanzisha pamoja na kuendeleza mradi huu wa elimu ni Ubunifu uliotumika na sio uchawi mpeni ushirikiano mkubwa .ameongeza Chalamila"
Nao baadhi ya wazazi waliohudhulia mahafali wameushukuru uongozi wa shule za Kemebos na Kaizirege kuendekea kuwalea na kuwapa elimu bora watoto wao huku wakiwashauri wazazi ,walimu na wanafunzi kuendelea kushirikiana kwa pamoja na kiendeleza maadili mema kwa jamii.
Ikumbukwe shule hiyo ilianzishwa mwaka 2007 mpaka sasa imetimiza miaka 17 huku wanafunzi waliohitimu kidato cha 6 wakiwa 146.
0 Comments