Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS DKt.HUSSEIN MWINYI AWEKA JIWE LA MSINGI LA UFUNGUZI WA SKULI YA MSINGI YA KIDONGO CHEKUNDU WILAYA YA MJINI UNGUJA

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiondoa pazia na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Mohamed Mussa, kuweka Jiwe la Msingi la Ufunguzi wa Skuli ya Msingi ya Kidongochekundu Wilaya ya Mjini Unguja leo 24-4-2023, na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 59 ya Muungano wa Zanzibar na Tanganyika.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi na Viongozi mbalimbali wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Mjini Unguja Mhe. Rashid Msaraka, akitowa maelezo ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ufunguzi wa Skulu ya Msingi ya Kidongochekundu Wilaya ya Mjini Unguja, ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 59 ya Muungano wa Zanzibar na Tanganyika .(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kulifungua Jengo Jipya la Skuli ya Msingi ya Kidongochekundu Wilaya ya Mjini Unguja iliyojengwa kupitia fedha za Uviko-19, ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 59 ya Muungano wa Zanzibar na Tanganyika na (kulia kwa Rais) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Lela Mohamed Mussa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Mohammed Said Dimwa na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mwanafunzi Hunaina Hamad wa Darasa la Saba wa Skuli ya Msingi ya Kidongochekundu , alipotembelea Maabara ya Sayansi ya Skuli hiyo baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Ufunguzi wa Skuli hiyo uliofanyika leo 24-4-2023, na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Mohammed Mussa na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrissa Kitwana Mustaf.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia wakati wa hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Skuli ya Msingi ya Kidongochekundu Wilaya ya Mjini Unguja, iliyojengwa kwa fedha za Uviko -19, uzinduzi huo uliofanyika leo 24-4-2023, ikiwa ni shamrashamra Maadhimisho ya Miaka 59 ya Muungano wa Zanzibar na Tanganyika.(Picha na Ikulu)
MUONEKANO wa Jengo jipya la Skuli ya Msingi ya Kidongochekundi Wilaya ya Mjini Unguja lililojengwa kwa fedha za Uviko -19.,. lililofunguliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha Miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.(Picha na Ikulu)

Post a Comment

0 Comments