*********************
Na mwandishi wetu Jeshi la Polisi-Dar es salaam
Team ya Judo ya Jeshi la Polisi imefanikiwa kutwaa ubingwa wa jumla wa mchezo wa Judo kwa mashindano ya shirikisho la wakuu wa Polisi afrika mashariki iliyofanyika Nchini Rwanda Kuanzia march 21 hadi 27 mwaka huu.
Akiongea leo April 13 2023 mara baada ya ukabidhi kikombe hicho kwa Mkuu wa chuo cha Polisi Dar es salaam kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Dkt Lazaro Mambosasa Kocha mkuu wa Team hiyo konstebo wa Polisi Zaidi khamisi amesema walijianda vyema na kudumisha nidhamu katika mchezo huo kitendo kilichopelekea kutwaa ushindi na kupata kikombe cha ushindi katika mashindano ya shirikisho la wa wakuu wa Polisi Nchini Rwanda.
Aidha kocha huyo amemshukuru Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP CAMILIUS WAMBURA kwa namna alivyowawekea mazingira mazuri katika maandalizi yao kuelekea mashindano hayo Nchini Rwanda ambapo umepelekea kuutwaa ubingwa huo.
Sambamba na hilo kocha huyo amemshukuru mkuu wa chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi Dkt Lazaro Mambosasa kwa kuwapa eneo la kufanya maandalizi ya mashindano yao katika chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA) kabla ya Kwenda kushiriki mashindano ya shirikisho la wakuu wa Polisi ukanda wa afrika mashariki yani Police EAPCCO GAMES ambayo yamefanyika nchini Rwanda na kuhusisha nchi.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Dkt. LAZARO MAMBOSASA amewapongeza na kuwashukuru askari hao walioshiriki vyema mashindano na kutwaa ubingwa huo.
Daktari Mambosasa amesema mbali na kutwaa ubingwa huo amesema kutwaa ubingwa huo ni kuitangaza nchi na Jeshi la Polisi kimataifa ambapo amewaomba kuendelea kushiriki kikamilifu kwa mashindano makubwa yajayo na kutwaa ubingwa.
0 Comments