Ticker

6/recent/ticker-posts

MIRADI YOTE IKAMILIKE KWA WAKATI – GUGU


Katibu Tawala Mkoa Bw. Ally Senga Gugu (Kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bahi Bw. Athumani Masasi kuhusu hatua ya ujenzi wa jengo la huduma za dharura katika Hospitali ya Wilaya ya Bahi jana tarehe 13/04/2023. Halmashauri ya Wilaya ya Bahi iko katika hatua za mwisho za ukamilishaji wa majengo 18 kati ya majengo 28 yanayotakiwa kwenye hospitali hiyo jumla ya Shilingi Bilioni 4.3 zimetumika
Katibu Tawala Mkoa Bw. Ally Senga Gugu (Kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Dkt. Honest Kasasa wa Hospitali ya Wilaya ya Bahi kuhusu huduma zilizoanza kutolewa katika Hospitali ya Wilaya ya Bahi jana tarehe 13/04/2023.
Katibu Tawala Mkoa Bw. Ally Senga Gugu (Kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bahi Bw. Athumani Masasi mara baada ya kufanya ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo katika Ujenzi wa Zahanati ya Nagulo Bahi ambapo ujenzi wake uko katika hatua za umaliziaji. Kituo hiki ni jitahada za wananchi waliohamasishana kuanza ujenzi mwaka 2019 na kuungwa mkono na Halmashauri ya Bahi.
Katibu Tawala Mkoa Bw. Ally Senga Gugu akikagua ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi Mpamantwa Barabarani ambapo ujenzi wake umekamilika ikiwa ni jitihada za wananchi na Serikali ya Kijiji ambapo ujenzi wake umegharimu kiasi cha Shilingi 38,893,980/=

*************************

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw. Ally Gugu amesema lengo na matarijio ya Mkoa nikuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa kuzingatia muda uliowekwa na viwango vya ubora unaotakiwa kwa kuzingatia thamani ya fedha.

Gugu ameyasema hayo leo tarehe 13/04/2023 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika Wilaya ya Bahi kwa lengo la kukagua utekezaji wa miradi ya maendeleo katika wilaya hiyo.

Gugu amehimiza watumishi wanaosimamia miradi hiyo kuwajibika na kuhakikisha usimamizi madhubuti wa miradi yote ya maendeleo na kutoa angalizo juu ya hatua zitakazochukuliwa dhidi ya miradi ambayo haitakamika kwa wakati na ubora unaotakiwa.

“Serikali ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeleta fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya afya na elimu katika Halmashauri zetu, tusiwe moja ya vikwazo katika kusimamia ukamilifu wa miradi hii, tunatoyaka kufanya yafanyike kwa wakati na hapa nisisitize kubwa zaidi kusiwe na viporo vya kutokamilika kwa miradi ya maendeleo. Sote tudhamirie kukamilisha kazi zote zilizopangwa kutekelezwa katika mwaka huu wa fedha kwa kuzingatia mpango kazi” Gugu alisisitiza.

Awali, Katibu Tawala Bw. Gugu alipata wasaa wa kuzungumza na Watumishi wa Wilaya ya Bahi na kuwataka kutumiza wajibu wao kwa kuzingatia Sheria, Taratibu na Kanuni za Utumishi wa Umma.

“Haki zinaenda sambamba na wajibu, hivyo timizeni wajibu wenu kikamilifu kila mmoja katika nafasi yake”

Halmashauri ya Wilaya ya Bahi iko katika hatua za mwisho za ukamilishaji wa majengo 18 kati ya majengo 28 yanayotakiwa kwenye hospitali ya Wilaya ambapo jumla ya Shilingi Bilioni 4.3 zimetumika.

Kutokana na kukamilika kwa baadhi ya majengo katika Hospitali hiyo imewezesha kuanzishwa kwa huduma ya mionzi, huduma ya upasuaji ambapo mpaka sasa akina mama 212 wamefanyiwa upasuaji, uwepo wa huduma za X-Ray na Ultrasound na kutoa huduma kwa watoto waliozaliwa chini ya umri kamili wa mimba yaani Watoto njiti.

Bw. Gugu katika ziara yake amekagua pia ujenzi wa Zahanati ya Nagulo, Shule ya Msingi Bahi English Medium Pre and Primary School, Shule ya Msingi Mpamantwa Barabarani na Shule ya Msingi Kigwe yenye wanafunzi wenye mahitaji maalumu.

Post a Comment

0 Comments