Ticker

6/recent/ticker-posts

KUPITIA KAMPENI YA BONGE LA MPANGO, MOTO ULE ULE YA NMB, DROO YACHEZESHWA NA KUPATA WASHINDI

Mkuu wa Idara ya Mauzo NMB Bw.Donatus Richard akizungumza katika ufunguzi na kuchezesha droo ya kwanza ya Kampeni ya 'BONGE LA MPANGO , MOTO ULE ULE' awamu ya tatu iliyofanyika leo Aprili 13,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Mauzo NMB Bw.Donatus Richard akizungumza katika ufunguzi na kuchezesha droo ya kwanza ya Kampeni ya 'BONGE LA MPANGO , MOTO ULE ULE' awamu ya tatu iliyofanyika leo Aprili 13,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Bw.Elibariki Sengasenga (kulia) akizungumza katika ufunguzi na kuchezesha droo ya kwanza ya Kampeni ya 'BONGE LA MPANGO , MOTO ULE ULE' awamu ya tatu iliyofanyika leo Aprili 13,2023 Jijini Dar es Salaam.


NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

BENKI ya NMB imefungua na kuchezesha droo ya kwanza ya Kampeni ya 'BONGE LA MPANGO , MOTO ULE ULE' na kuwapata washindi ambao wamejishindia pikipiki pamoja na fedha tasilimu ya shilingi laki mbili kila mmoja.

Katika ufunguzi wa Kampeni hiyo ambayo imefanyika leo Aprili 13,2023 katika Makao Makuu ya NMB Jijini Dar es Salaam, wametangazwa washindi wawili kutoka maeneo tofauti ambao ni Stella Meleck Mafuwe kutoka Babati ambaye amejishindia pikipiki ya shilingi milioni tatu na wa pili ni Mushema Deocles Muganyizi kutoka Mwanza ambaye amejinyakulia pesa tasilimi shilingi laki mbili.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ufunguzi wa kampeni hiyo, Mkuu wa Idara ya Mauzo NMB Bw.Donatus Richard amesema zawadi ambazo waliziandaa kwa wateja watakaofungua na kuweka akiba kwenye Benki ya NMB kuanzia shilingi Laki moja (100,000/=) nakuendelea kunafaida ambazo atajishindia ikiwemo pesa taslimu, pikipiki ya miguu mitatu, pikipiki za miguu miwili pamoja, friji ya milango miwili, TV janja, Simu ya mkononi, Laptop, mashine ya kufulia nguo na zawadi nyingine nyingi.

Amesema Kampeni hii ya Bonge la Mpango awamu ya tatu inajumuisha wateja wote wa NMB kwa sasa na wale watakaofungua akaunti mpya ya NMB.

"Hata hivyo kwenye Kampeni hii kutakuwa na zaidi ya shilingi milioni 180 zitakazotolewa kama zawadi kwa washindi 100 lakini pia kwenye kampeni hiyo itakayoendeshwa ndani ya wiki 12 kila wiki tutapata washindi 12 watakaopokea shilingi laki moja kila mmoja pia kutakuwa na mshindi mmoja kila wiki atakaejishindia shilingi laki mbili na vilevile kutakuwa na mshindi kila wiki atakaekuwa anajishindia pikipiki". Amesema

Aidha amesema Washindi watano watajinyakulia shilingi milioni moja kwa kila mwezi kwa kila mtu na katika kuhitimisha kampeni hiyo kwenye fainali watakuwa na washindi 11 watakaojumuisha vitu vifuatavyo kama pikipiki, bajaji za mizigo na wengine 7 watajishindia vifaa vya kielektroniki kama friji ya milango miwili, TV janja, Simu janja za Iphone 14, laptop na mashine za kufulia nguo .

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Bw.Elibariki Sengasenga ameipongeza NMB kwa kuandaa kampenihiyo kwani toka mwanzo wamekuwa wakitoa ushirikiano mzuri mpaka hadi sasa kuelekea kampeni ya Bonge la Mpango.

Pamoja na hayo amewataki ushiriki mwema wale wote watakaoshiriki kwenye kampeni hiyo ambayo imeanza na kuwapata washindi ambao watapewa zawadi zao.

Post a Comment

0 Comments