NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma PIC, imeishauri Serikali kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Taasisi mbalimbali nchini katika kutekeleza miradi mbalimbali ili kuhakikisha miradi ambayo wanaisimamia iweze kuisha kwa wakati.
Wito huo umetolewa leo na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe.Jerry Silaa Wakati walipotembelea Miradi inayosimamiwa na Shirika la Nyumba la Taifa NHC Jijini Dar es Salaam, ambapo wametembelea mradi wa Morocco Square, Mradi 7/11 uliopo kawe pamoja na Mradi wa Samia Housing Scheme uliopo tanganyika Packers Kawe Jijini Dar es salaam.
Amesema Mashirika ya umma yameundwa kufanya kazi ya kutengeneza faida kwa kuhakikisha wanafanya mipango ili kufikia malengo waliojiwekea kama miradi ya Morroco square na 7/11 ambayo imegharimu Taifa.
"Shirika la nyumba NHC ni Shirika mkombozi kwa makazi ya mtanzania kwakuwa wamekuwa wakirahisha kwenye ujenzi wa nyumba ambapo unanunua nyumba ambayo imeshajengwa tayari na kuokoa muda wa kusimamia ujenzi" amesema Mhe.Jerry.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa ( NHC) Bw. Hamad Abdallah, ameishukuru kamati ya bunge hiyo kwakutenga muda wao na kuthamini majukumu ambayo wamepewa na taifa ya kusimamia mashirika ambayo yanafanya uwekezaji.
Amesema mradi wa Morocco Square umekamilika kwa asilimia 97 na muda si mrefu wataruhusu wapangaji, na Mradi wa Samia Housing Scheme unaendelea na ujenzi na wanatarijia kumaliza mwisho wa mwaka huu wenye nyumba takribani 560 na wanunuzi wameshapata kwa asilimia 80.
Aidha amemuhakikishia Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma PIC kusimamia miradi hiyo kwa gharama sahihi ikiwemo vifaa kuchukua moja kwa moja kutoka viwandani.

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
0 Comments