Afisa kutoka Wizara ya Afya Zanzibar Hafidh Abdurahman Seif akizungumza na kikundi cha Wagonjwa wa Maradhi yasioambukiza wakati alipokua akitoa elimu juu ya maradhi hayo kabla ya kuanza kwa zoezi la utoaji wa huduma za Afya ngazi ya jamii lililoandaliwa na Wizara ya Afya wakishirikiana na PharmAccess international huko Koani Wilaya ya Kati .PICHA NA FAUZIA MUSSA -MAELEZO ZANZIBAR
Mwana kikundi cha Wagonjwa wa Maradhi yasioamhmbukiza Bimkasi akizungumza wakati alipokua Akitoa ushuhuda wa mabadiliko ya Afya yake mara baada ya kufanya mabadiliko ya mlo, wakati wa zoezi la utoaji wa huduma za Afya ngazi ya jamii lililofanyika Koani Wilaya ya kati.PICHA NA FAUZIA MUSSA -MAELEZO ZANZIBAR
Maafisa wa Afya walipokuwa wakitoa huduma za Afya katika ngazi ya Jamii kwa Wagonjwa wa Maradhi yasioambukiza huko Koani Wilaya ya Kati Mkoa wa Kaskazini Unguja .PICHA NA FAUZIA MUSSA -MAELEZO ZANZIBAR
********************
Na Fauzia Mussa -Maelezo Zanzibar
Jamii imeshauriwa kutumia mlo uliokamiki ili kuepuka maradhi yasioambukiza ambayo yameshika kasi katika jamii.
Ameyasema hayo Afisa kutoka Wizara ya Afya Zanzibar Hafidh Abdurahman Seif wakati alipokua akitoa elimu kwa wagonjwa wa maradhi yasioambukiza katika hafla ya wa utoaji wa huduma za Afya kwa ngazi ya jamii huko Koani Wilaya ya Kati Unguja
Ameeleza kuwa maradhi ya kuambikiza yamekua yakiongezeka kwa kasi zaidi kutokana na jamii kutokuwa tayari kufanya mabadiliko ya mfumo wa chakula
Alisema ulaji usiozingatia makundi ya mlo ni sababu inayopelekea maradhi hayo kuongezeka hivyo ameishauri jamii kupunguza matumizi ya vyakula vya uwanga na kutumia matunda kwa wingi.
"Nibora Kula chakula Bora nasio Bora chakula, tuachane na vyakula vya kusindikwa vimekosa virutubisho ,sasa tutumie vyakula vyetu vyaasili ambayo hata gharama yake nindogo"alishauri
Alifahamisha kuwa kiafya kwa siku inatakiwa kutumia uwanga ujazo wa mkono , mboga mboga kwa wingi na mafuta yasiozidi vijiko viwili vya chakula hivyo ameiasa jamii kuwa na Utamaduni huo ili kupunguza ongezeko la maradhi hayo.
"Kitu chochote kinapoongezeka katika mwili ni sumu, si uwanga,mafuta ,sukari wala chumvi ivyo tujitahii kupunguza matumizi ya vitu hivi kwani ni miongoni mwa sababu za maradhi haya"alifahamisha
Aliongeza kuwa maradhi yasioambukiza yamekua yakiendelea kuongezeka siku Hadi siku kutokana na jamii kutokua tayari kuachana na matumizi ya vichocheo vya maradhi hayo sambamba na urithi kutoka kwa familia.
Aidha amefahamisha kuwa uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe kupitiliza umetajwa kusababisha maradhi yasioambukiza ikiwemo pumu na saratani ya mapafu .
Afisa huyo ameeleza kuwa jamii haina mazowea ya kufanya mazoezi ya viungo jambo ambalo linasababisha ongezeko la wagonjwa wa maradhi hayo siku hadi siku.
Amesema mazoezi ni njia moja wapo ya kutoa takataka mwilini hivyo ni vyema kufanya mazoezi ya viungo angalau nusu saa kwa siku kwani kutasaidia kupunguza ongezeko la maradhi hayo
Hata hivyo Afisa huyo aliishauri jamii kujitokeza katika vituo vya Afya kufanyiwa vipimo mara kwa mara ili kuangalia Afya zao dhidi ya maradhi yasioambukiza .
Nao waathirika wa maradhi yasioambukiza wameishukuru Wizara ya Afya na Pharm Access kwa kuwafikia na kuwapatia elimu juu ya maradhi hayo sambamba na kuwasogezea huduma za Afya katika ngazi ya jamii.
"Tangu nipate muamko na elimu nimebadilika nakunywa uji wa mtama saa Saba nakula dona ,mboga na supu ya dagaa,usiku nakula mkate wa atta nikikosa narudia uji basi alhamdulillah kwa sasa naendelea vizuri nafika shamba kulima"alielezea Bimkasi miongoni mwa wagonjwa wa sukari.
0 Comments