WASHINGTON
Shirika la Fedha la Kimataifa IMF Aprili 24, 2023 limeidhinisha mkopo wa dola milioni 153 kwa Tanzania.
Taarifa ya Shirika hilo iliyotolewa muda mfupi uliopita imesema kuwa bodi ya wakurugenzi ya Shirika hilo ilipitia na kuridhishwa na mpango wa miaka mitatu wa serikali ya Tanzania katika kusimamia uchumi pamoja na kukabiliana na madeni.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa IMF Antoinette Sayeh amesema mpango wa mabadiliko ya kiuchumi nchini Tanzania unaendelea vizuri pamoja na kukabiliana na changamoto za kiuchumi duniani.
“Utekelezaji wa mipango yote umekuwa imara, vigezo vyote vya malengo ya Disemba 2022 vimekamilishwa na mawili kati ya matatu yalipangwa mpaka ifikapo Disemba 2022 yamekilika katika muda uliyopangwa” alisema.
Hata hivyo amesema serikali ya Tanzania bado inatakiwa kuongeza juhudi katika kukusanya mapato ya ndani na kuchukua hatua za kufanya mabadiliko ya kimuundo ili kuondoa urasimu na kuzuia vitendo vya rushwa.
Antoinnete amesema kwa Tanzania kuimarisha ukusanyaji wa napata ya ndani na kuzuia matumizi holela ya fedha kutasaidia serikali kuboresha miradi ya kijamii na wakati huo huo kukabiliana vizuri na deni lake.
Amesema hatari ya Tanzania kutumbukia katika matatizo ya madeni ni ya kiwango cha kati, lakini ni muhimu kuendelea kutoa kipaumbele kwenye mikopo ya riba nafuu na kuhakikisha kuwa hatari zinzoweza kutokea kutokana na madeni zinadhibitiwa.
Hatua hiyo ya IMF inafanya kiasi kilichotolewa kwa Tanzania katika ombi la
mkopo wa dola bilioni 1.04, kufikia kiasi cha dola milioni 304.
Chanzo; Moonlight
0 Comments