Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dkt. John Luzila (kushoto) akipokea Vifaa vya kufanyia upasuaji wa mifupa mirefu kwa ajili ya Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga imetangaza kuanza kutoa huduma mpya ya Upasuaji wa mifupa ambayo kwa muda mrefu wananchi wa Shinyanga wamekuwa wakihangaika wanapopata changamoto ya kuvunjika kwa mifupa na kulazimika kusafiri kwenda katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando Jijini Mwanza.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Ijumaa Aprili, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dkt. John Luzila amesema kupitia urafiki wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga na Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma wamepata udhamini wa vifaa kwa ajili ya Operesheni ya mifupa kupitia Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma kwa ufadhili wa SIGN Fracture Care International.
"Kupitia huduma hii tulipata madaktari bingwa wawili kutoka Hospitali ya Rufaa Dodoma ambao tumekuwa nao tangu Aprili 17,2023 mpaka leo kwa ajili ya kuona wagonjwa wenye shida au changamoto ya mifupa na wengine pia wamefanyiwa Operesheni lakini pia kuwajengea watumishi wenzetu wa Hospitali ya Rufaa Shinyanga kuwa na uwezo wa kufanya hizo Oparesheni za mifupa.
Sambamba na hayo tuna Daktari wetu Bingwa tulimtuma Hospitali ya Rufaa ya Dodoma ambaye amekaa kwa muda wa mwezi mzima kwa ajili ya kujijengea uwezo wa kufanya Oparesheni za mifupa", amesema Dkt. Luzila.
Dkt. Luzila ameishukuru sana Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya upatikanaji wa huduma hiyo ya oparesheni ya mifupa katika hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga ili kupunguza changamoto ya wagonjwa kupelekwa Bugando
"Vifaa hivi tulivyopata tumepata seti moja ambayo ina uwezo wa kuhudumia wagonjwa 28 kwa sasa hivi na kadri vifaa vitakavyokuwa vikitumika tutakuwa tunaomba vingine kwa ajili ya kuendeleza huduma hii ya upasuaji wa mifupa",amesema Dkt. Luzila.
Kwa upande wake, Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Mifupa Dkt. Hamis Paul Mpigahodi ambaye ni Mkuu wa Idara ya Upasuaji katika Hospitali ya Rufaa Mkoawa Shinyanga amesema sasa wakazi wa Shinyanga watanufaika na huduma ya upasuaji wa mifupa badala ya kutumia muda mwingi na gharama kusafiri kwenda Bugando kupata huduma hiyo.
Naye Daktari Bingwa wa Mifupa kutoka Hospitali ya Rufaa Dodoma, Dkt. Lusekelo William akizungumza wakati wa kukabidhi Vifaa vya kufanyia upasuaji wa mifupa mirefu kwa ajili ya Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga amewaomba wananchi wa mkoa wa Shinyanga kufika katika hospitali ya rufaa Mkoa wa Shinyanga kupata huduma hiyo kwa watoto na watu wazima hakuna madhara na vyuma vinatolewa mfupi baada ya mgonjwa kupona.
Nao baadhi ya wagonjwa walionufaika na huduma hiyo ya upasuaji akiwemo bi. Sinzo Ongalla na bw. Lotih Nkango wameishukuru Serikali kusogeza karibu huduma ya upasuaji badala ya kusafiri kwenda Bugando kupata huduma hiyo.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dkt. John Luzila akielezea kuhusu huduma mpya ya Upasuaji wa mifupa mirefu katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dkt. John Luzila akielezea kuhusu huduma mpya ya Upasuaji wa mifupa mirefu katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga.
Daktari Bingwa wa Mifupa kutoka Hospitali ya Rufaa Dodoma, Dkt. Lusekelo William akielezea kuhusu huduma mpya ya Upasuaji wa mifupa mirefu katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga.
Daktari Bingwa wa Mifupa kutoka Hospitali ya Rufaa Dodoma, Dkt. Lusekelo William akielezea kuhusu huduma mpya ya Upasuaji wa mifupa mirefu katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga.
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Mifupa Dkt. Hamis Paul Mpigahodi ambaye ni Mkuu wa Idara ya Upasuaji katika Hospitali ya Rufaa Mkoawa Shinyanga akielezea kuhusu huduma mpya ya Upasuaji wa mifupa mirefu katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga.
Vifaa vya kufanyia upasuaji wa mifupa mirefu kwa ajili ya Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga
Vifaa vya kufanyia upasuaji wa mifupa mirefu kwa ajili ya Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dkt. John Luzila (kushoto) akipokea Vifaa vya kufanyia upasuaji wa mifupa mirefu kwa ajili ya Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dkt. John Luzila (kushoto) akipokea Vifaa vya kufanyia upasuaji wa mifupa mirefu kwa ajili ya Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dkt. John Luzila (kushoto) akipokea Vifaa vya kufanyia upasuaji wa mifupa mirefu kwa ajili ya Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga
Bi. Sinzo Ongalla mmoja wa wakazi wa Shinyanga walionufaika na huduma ya upasuaji mifupa akiishukuru Serikali kusogeza karibu huduma ya upasuaji mkoani Shinyanga badala ya kusafiri kwenda Bugando Jijini Mwanza kupata huduma hiyo.
Bw. Lotih Nkango mmoja wa wakazi wa Shinyanga walionufaika na huduma ya upasuaji mifupa akiishukuru Serikali kusogeza karibu huduma ya upasuaji mkoani Shinyanga badala ya kusafiri kwenda Bugando Jijini Mwanza kupata huduma hiyo.
Muonekano wa picha ya mfupa uliovunjika kabla ya kufanyiwa upasuaji
Muonekano wa picha ya mfupa uliovunjika baada ya kufanyiwa upasuaji
Muonekano wa picha ya mfupa uliovunjika baada ya kufanyiwa upasuaji
0 Comments