Ticker

6/recent/ticker-posts

FAMILIA YA GULAM HAFEEZ MUKADAM YATOA ZAWADI MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI KWA WATOTO BUHANGIJA

Familia ya Diwani wa kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga Mhe. Gulam Hafeez Mukadam (kulia) ikikabidhi chakula katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Katika Muendelezo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Familia ya Diwani wa kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga Mhe. Gulam Hafeez Mukadam imetoa zawadi ya chakula katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum (Wasioona, Viziwi na wenye ulemavu wa ngozi) cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vyakula hivyo, leo Jumatano Aprili 5,2023, Diwani wa kata ya Mjini Shinyanga Mhe. Gulam Hafeez Mukadam amesema familia yake imefika katika kituo hicho cha Buhangija kwa ajili ya kupeleka sadaka kwa watoto hao wenye mahitaji maalum.

“Tupo kwenye mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, tumekuja hapa kuleta sadaka hii kwa niaba ya wafadhili wetu waliopo Marekani kwa ajili ya kuleta chakula kwa watoto wetu katika kituo cha Buhangija”,ameeleza Mukadam.

Amevitaja vyakula hivyo kuwa ni Mchele kilo 50, unga wa sembe kilo 30, sukari kilo 25, unga wa ngano kilo 25,mafuta ya kupikia lita 10,maharage kilo 25, chumvi pakti 1, sabuni ya unga kilo 25, sabuni za vipande boksi 1,nyama kilo 10, viazi kilo 10, tambi boksi moja vyote vikiwa na thamani ya shilingi 700,000/=.
“Tunawashukuru wadau walioungana na familia yetu kutupatia msaada kwa ajili ya watoto hawa ambao nimekuwa mdau wa muda mrefu nikiwa miongoni mwa waanzilishi wa kituo hiki. Wito wangu ni kwa wadau mbalimbali tuwe mfano wa kuwakumbuka watoto hawa kwani ni watoto wote sote”,amesema Mukadam.

Gulam pia ametoa wito kwa Taasisi mbalimbali na jamii kwa ujumla kujenga utamaduni wa kuwasaidia mara kwa mara watoto hao ambao kwa sehemu kubwa wanatoka katika familia duni na wengine ni yatima hasa ikizingatiwa kuwa mahitaji yao ya kila siku ni makubwa.

Kwa upande wake, Mke wa Mhe. Gulam Hafeez Mukadam Bi. Mehrunnissa Allimia Chilwan maarufu Anti Meru amewataja wafadhili waliofanikisha kupatikana kwa vyakula kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalum Buhangija kuwa ni ndugu Nisha Kumar, Sumairah Toor,Zehra Toor, Anjum Toor, Nabeel Siddiqui na Farjana Chilwan.

Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Buhangija Jumuishi, Bi. Rose Daudi amewashukuru wadau hao kwa kusaidia watoto hao huku akimpongeza na kumshukuru Mhe. Gulam Hafeez Mukadam kwa kuendelea kuwa karibu na kituo cha Buhangija na kufanikisha kupatikana kwa mahitaji mbalimbali katika kituo hicho ambacho sasa kina jumla ya watoto 201 wenye ulemavu wa ngozi, viziwi na wasiosikia.

Nao watoto hao wameishukuru familia ya Mzee Gulam Hafeez Mukadam kwa kuwapatia msaada huo na kuomba wadau wengine kuendelea kufika katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum.

Katika hatua nyingine Diwani huyo wa kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga Mhe. Gulam Hafeez Mukadam amekabidhi msaada wa mifuko mitatu ya saruji kwa Mjasiriamali Alafat Ntemanya mkazi wa Mtaa wa Viwandani Mjini Shinyanga kwa ajili ya kuboresha kibanda cha kuoneshea michezo kinachojulikana kwa jina la Home and Away Sports Arena kilichopo Nguzo Nane Mjini Shinyanga.
Diwani wa kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga Mhe. Gulam Hafeez Mukadam akizungumza katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum (Wasioona, Viziwi na wenye ulemavu wa ngozi) cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Diwani wa kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga Mhe. Gulam Hafeez Mukadam akizungumza katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum (Wasioona, Viziwi na wenye ulemavu wa ngozi) cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga.
Mke wa Diwani wa kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga Mhe. Gulam Hafeez Mukadam Bi. Mehrunnissa Allimia Chilwan maarufu Anti Meru akizungumza katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga.

Familia ya Diwani wa kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga Mhe. Gulam Hafeez Mukadam Bi. Mehrunnissa Allimia Chilwan maarufu Anti Meru na wageni mbalimbali wakiwa katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga.
Vyakula mbalimbali vilivyotolewa na familia ya Diwani wa kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga Mhe. Gulam Hafeez Mukadam kwa ajili ya watoto wanaolelewa kwenye kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga.
Familia ya Diwani wa kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga Mhe. Gulam Hafeez Mukadam Bi. Mehrunnissa Allimia Chilwan maarufu Anti Meru na wageni mbalimbali wakiwa katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga.
Familia ya Diwani wa kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga Mhe. Gulam Hafeez Mukadam (kulia) ikikabidhi sadaka ya vyakula katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga.
Familia ya Diwani wa kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga Mhe. Gulam Hafeez Mukadam (kulia) ikikabidhi chakula katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga.
Familia ya Diwani wa kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga Mhe. Gulam Hafeez Mukadam (kulia) ikikabidhi chakula katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga.
Familia ya Diwani wa kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga Mhe. Gulam Hafeez Mukadam (kulia) ikikabidhi chakula katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga.
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Buhangija Jumuishi, Bi. Rose Daudi akitoa neno la shukrani
Mwanafunzi akitoa neno la shukrani
Familia ya Diwani wa kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga Mhe. Gulam Hafeez Mukadam wakipiga picha ya pamoja na sehemu ya watoto katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga.
Diwani wa kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga Mhe. Gulam Hafeez Mukadam akizungumza na watoto wenye mahitaji maalum cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga.
Diwani wa kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga Mhe. Gulam Hafeez Mukadam akizungumza na watoto wenye mahitaji maalum cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga.
Diwani huyo wa kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga Mhe. Gulam Hafeez Mukadam akizungumzma wakati akikabidhi msaada wa mifuko mitatu ya saruji kwa Mjasiriamali Alafat Ntemanya mkazi wa Mtaa wa Viwandani Mjini Shinyanga kwa ajili ya kuboresha kibanda cha kuoneshea michezo kinachojulikana kwa jina la Home and Away Sports Arena kilichopo Nguzo Nane Mjini Shinyanga.
Mjasiriamali Alafat Ntemanya mkazi wa Mtaa wa Viwandani Mjini Shinyanga akizungumza wakati akipokea mifuko ya saruji kutoka kwa Diwani wa kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga Mhe. Gulam Hafeez Mukadam kwa ajili ya kuboresha kibanda cha kuoneshea michezo kinachojulikana kwa jina la Home and Away Sports Arena kilichopo Nguzo Nane Mjini Shinyanga.
Diwani wa kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga Mhe. Gulam Hafeez Mukadam  (wa pili kulia) akikabidhi msaada wa mifuko mitatu ya saruji kwa Mjasiriamali Alafat Ntemanya  (wa pili kushoto) mkazi wa Mtaa wa Viwandani Mjini Shinyanga kwa ajili ya kuboresha kibanda cha kuoneshea michezo kinachojulikana kwa jina la Home and Away Sports Arena kilichopo Nguzo Nane Mjini Shinyanga.

Mifuko mitatu ya saruji iliyotolewa na Diwani wa kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga Mhe. Gulam Hafeez Mukadam kwa Mjasiriamali Alafat Ntemanya  mkazi wa Mtaa wa Viwandani Mjini Shinyanga kwa ajili ya kuboresha kibanda cha kuoneshea michezo kinachojulikana kwa jina la Home and Away Sports Arena kilichopo Nguzo Nane Mjini Shinyanga.
Muonekano wa sehemu ya kibanda cha kuoneshea michezo kinachojulikana kwa jina la Home and Away Sports Arena kilichopo Nguzo Nane Mjini Shinyanga.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Post a Comment

0 Comments