Mkuu wa Wilaya ya Kusini Mhe. Rajab Mkasaba ameongoza zoezi la kutoa elimu juu ya matumizi ya nishati safi kwa watoa huduma wa ngazi ya jamii 100 wa Wilaya ya Makunduchi.
Zoezi hilo liliambatana na kugawa mitungi 100 ya Oryx ambapo Doris Mollel Foundation @dorismollelfoundation)kwa kushirikiana na Oryx Energies Tanzania (@oryxenergiestanzania) wameweka nia ya kuwafikia watoa huduma 1000 nchini.
Mkuu wa Wilaya hiyo alisema anashukuru sana kwa jitihada zilizofanywa na Taasisi hizi mbili kwa kufawikia watoa huduma za afya ngazi ya jamii katika Wilaya yake na ametoa rai kwa watoa huduma hao kua mabalozi kwa watu wengine juu ya matumizi sahihi ya nishati salama.
Mganga Mkuu wa hospitali ya Makunduchi Dr. Mohamed Mnyimbi alishukuru sana Taasisi hizi mbili na kupongeza jitihada za kusaidia afya ya Mama na mtoto iliyofanywa na Taasisi hizo kuanzia shughuli ya Taarab kwa watoto njiti iliyofanyika Mwezi wa Tatu mwaka huu hadi zoezi hili.
0 Comments