Bodi ya Wakurugenzi ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ikiongozwa na Mwenyekiti wake ambaye pia ni Gavana wa BoT, Bw. Emmanuel Tutuba, imefanya ziara Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) na Shirika la Reli Tanzania(TRC) kujionea uendeshwaji wa shughuli za kiuchumi na uwekezaji uliofanywa na serikali katika sekta hiyo ya usarifishaji.
Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Mrisho S. Mrisho, akifafanua jambo kwa Bodi ya Wakurugenzi ya BoT iliyoongozwa na Gavana, Bw. Emmanuel Tutuba katika ziara ya Bodi hio ambapo wamejionea namna bandari hio inaendeshwa.
Bodi ya Wakurugenzi ya BoT iliyoongozwa na Gavana, Bw. Emmanuel Tutuba, wakitazama reli ya kisasa (SGR) katika stesheni iliyopo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Shirika la Reli Tanzania (TRC), Bw. Senzige Kisenge, akifafanua jambo kwa Bodi ya Wakurugenzi ya BoT iliyoongozwa na Gavana, Bw. Emmanuel Tutuba kuhusu jengo la stesheni ya reli ya kisasa (SGR) lilipo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Shirika la Reli Tanzania (TRC), Bw. Senzige Kisenge, akitoa maelezo kwa Bodi ya Wakurugenzi ya BoT iliyoongozwa na Gavana, Bw. Emmanuel Tutuba, kuhusu namna chumba cha uendeshaji kitatumika katika kusimamia kazi za SGR.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari, Bw. Plasduce Mkeli Mbossa, akifafanua jambo kwa Gavana wa BoT, Bw. Emmanuel Tutuba wakati wa ziara ya Bodi ya Wakurugenzi ya BoT iliyofanyika kwenye bandari ya Dar es Salaam, kujionea namna shughuli za kiuchumi zinaendeshwa katika bandari hio.
Gavana wa BoT, Bw. Emmanuel Tutuba, akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari, Bw. Plasduce Mkeli Mbossa, katika ziara ya Bodi ya Wakurugenzi ya BoT iliyofanyika kwenye bandari ya Dar es Salaam, kujionea namna shughuli za kiuchumi zinaendeshwa katika bandari hio.
0 Comments