Ticker

6/recent/ticker-posts

BENKI YA I&M TANZANIA INALENGA UKUAJI THABITI NA UFANISI WA BIASHARA KWA MWAKA 2023

Benki ya I&M Group PLC ilipata faida ya KES11.6 bilioni baada ya kodi kukatwa kwa mwaka mzima unaoishia Desemba 2022, ikiwa ni ongezeko la asilimia 34 la faida kutoka KES8.6 bilioni iliyopatikana katika kipindi kama hicho mwaka 2021. Matokeo hayo yalitangazwa Jijini Nairobi nchini Kenya, hivi karibuni na kusambazwa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Benki hiyo imesema ukuaji huo wa kuvutia umetokana na utekelezaji wa mafanikio unaendelea wa mkakati wake wa iMara 2.0, ambao kwa sasa uko katika mwaka wake wa 3 na wa mwisho, unaolenga ukuaji wa biashara, ufanisi wa uendeshaji, kuzingatia wateja na mabadiliko ya kidigitali.

Kutokana na utendaji kazi mzuri, Bodi ilipendekeza mgao wa jumla wa KES2.25 kwa kila hisa, ikiwa ni ongezeko la asilimia 50 kutoka mwaka jana, na kuleta jumla ya malipo ya gawio kuwa KES 3.7 bilioni na mavuno ya mgao wa asilimia 13.

I&M Group ilitambua ukuaji mzuri wa nambari za juu uliofanywa na Benki ya I&M Tanzania kutokana na ongezeko kubwa la amana na mikopo ya wateja. Mikopo Halisi na ya Awali ilikua kwa asilimia 6 hadi TZS366 bilioni kutoka TZS345 bilioni mwaka 2021 kutokana na mikopo ya kikampuni, rehani na kidijitali.

Amana za wateja wa benki zilikua kwa asilimia 37 hadi TZS 450 bilioni kutoka TZS 329 bilioni mwaka uliotangulia, uliotokana na wateja rejareja na makampuni. Mapato Halisi ya Riba yaliongezeka kwa asilimia 26 hadi TZS 31.8 bilioni kutoka TZS 25.3 bilioni mwaka uliotangulia na Mapato Yasiyogharimiwa yaliongezeka kwa asilimia 24 hadi TZS 11.6 bilioni kutoka TZS 9.4 bilioni mwaka 2021.

Licha ya hasara ambayo Benki ya I&M Tanzania ilipata mwaka 2022, Benki hiyo kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, iliripoti kuimarika kiutendaji kazi, ambapo jumla ya mali ziliongezeka kwa asilimia 17 mwaka 2022 hadi TZS 597 bilioni kutoka TZS511 bilioni mwaka uliotangulia.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya I&M Tanzania Bw. Zahid Mustafa, wakati akizungumzia kuhusu utendaji wa Benki hiyo, alisema “Hasara iliyoripotiwa ya TZS 13.5 bilioni mwaka 2022 kwa Benki ya I&M Tanzania ilitokana na uamuzi wa kufuta Mikopo Isiyolipika (Non-Performing Loans) kwa kuzingatia miongozo ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

“Mikopo Isiyolipika ilisababishwa na athari za janga la Ugonjwa wa Uviko-19, mfumuko wa bei duniani na athari ngumu ya mazingira ya uendeshaji kwa wateja wetu. Hii ilisababisha kuongezeka kwa utoaji wa mikopo kutoka TZS 5.2 billioni mwaka 2021 hadi TZS 25.3 billioni mwaka 2022.”

Bw. Mustafa ambaye alijiunga na Benki ya I&M Tanzania mwishoni mwa mwaka jana, alieleza zaidi kuwa Benki hiyo ina mipango wa kubadilisha biashara zake kwa kuanzisha mapendekezo tofauti ya rejareja na kidijitali ya kibenki kwa wateja wake nchini Tanzania, kuboresha uzoefu wa wateja, kuongeza ufanisi wa utendaji kazi na kupanua wigo wa wateja kuongeza ukuaji, ambao unahitaji uwekezaji mkubwa kwa watu na teknolojia.

Kufanikisha hilo, I&M Group PLC limeingiza mtaji wa dola za Kimarekani milioni 6 katika nusu ya kwanza ya Mwaka wa Fedha wa 2023. Bw. Mustafa alisisitiza kuwa Benki ya I&M itaendelea kujitolea kwa wateja wake na nchi kwa ujumla ikiwa na misingi mizuri ya biashara inayotokana na mkakati wa iMara 2.0 wa I&M Group PLC wa kukuza ukuaji, unaoendana na mizania yake thabiti ya kibiashara na muundo wa mtaji.

"Benki inatii masharti ya udhibiti na inabaki ikijiamini kwamba mkakati wake utaendelea kutoa matokeo bora kwa wateja na wanahisa wake sasa na siku zijazo," alisema Bw. Mustafa.

"Tuko mbioni kuzindua bidhaa mpya za biashara za kishirika na kirejareja kama vile ufufuaji wa utoaji mapendekezo kwa wafanyakazi wetu na majukwaa ya kidijitali ikiwemo uanzishwaji wa jukwaa la wakala la kibenki linaloitwa 'WAKALA'," alisema.

Katika miaka mitano ijayo, Benki ya I&M inatarajia kuwa mkopeshaji wa daraja la kwanza kwa kuendeshwa na ukuaji sawia unaochagizwa na ukuaji wa faida katika msingi wa wateja, upanuzi wa bidhaa na ufanisi wa uendeshaji.

Matumaini ya Benki ya I&M (TZ) yanachangiwa na uwezo wa jumla wa sekta ya benki katika Afrika Mashariki na ukuaji unaotia matumaini kutokana na mvuto wa sekta hiyo. Kuongezeka kwa ushindani ni ushahidi wa uwezekano wa ukuaji wa ziada na kwamba uwekezaji ni salama na utajiri wa kiuwekezaji unalindwa.


Kuhusu I&M

Benki ya I&M Tanzania ni mojawapo ya benki za biashara zinazokuwa kwa kasi, zinazotoa huduma mbalimbali za Kibenki kwa Mashirika, Biashara, Malipo, na Kibinafsi.

Ikiwa na makao yake makuu Dar es Salaam, Benki ya I&M Tanzania ni kampuni tanzu ya I&M Group PLC ambayo imeorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Nairobi na ina ukuwaji wa uwepo kikanda kwa sasa hadi katika nchi za Mauritius, Rwanda, Kenya, na Uganda. Imepewa leseni na Benki Kuu ya Tanzania. Benki ilianza kutoa huduma zake nchini Tanzania mwaka 2002 kama CF Union Bank.

Mnamo Septemba 2010, benki ilibadilisha jina lake kutoka CF Union Bank na kuwa I&M Bank (Tanzania) Limited, ili kuonyesha umiliki mpya. Kwa sasa benki hiyo inajiendesha katika majiji makubwa ikiwemo Dar es Salaam, Arusha, Mwanza and Kilimanjaro ikiwa na mipango ya kuendelea kutoa huduma mikoa mingine.

Benki ya I&M Tanzania inapigania kuwa Mshirika Anayeongoza wa Kifedha wa Ukuwaji kwa kutoa masuluhisho ya kibenki yanaendeshwa kiubunifu na kimasoko kwa ajili ya sehemu zake zilizolengwa.

Kwa taarifa zaidi tembelea tovuti yake www.imbank.com/tz
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya I&M Tanzania Bw. Zahid Mustafa.

Post a Comment

0 Comments