Kaimu Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Utekelezaji wa Sheria NEMC, Bw.Thobias Mwesiga akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya ukaguzi kwenye kiwanda bubu cha kukusanya na kusaga chupa za plastiki katika eneo la Kisarawe II wilayani Kigamboni leo Aprili 5,2023 Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Maafisa kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakitazama baadhi ya taka za hospitalini zikiwa zimekusanywa katika kiwanda bubu cha kukusanya na kusaga chupa za plastiki eneo la Kisarawe II wilayani Kigamboni leo Aprili 5,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa Maafisa kutoka NEMC akikagua baadhi ya taka za hospitalini zikiwa zimekusanywa katika kiwanda bubu cha kukusanya na kusaga chupa za plastiki eneo la Kisarawe II wilayani Kigamboni leo Aprili 5,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa Maafisa kutoka NEMC akikagua baadhi ya taka za hospitalini zikiwa zimekusanywa katika kiwanda bubu cha kukusanya na kusaga chupa za plastiki eneo la Kisarawe II wilayani Kigamboni leo Aprili 5,2023 Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya taka za hospitalini ambazo zimekutwa katika kiwanda bubu cha kukusanya na kusaga chupa za plastiki eneo la Kisarawe II wilayani Kigamboni leo Aprili 5,2023 Jijini Dar es Salaam.
Meneja wa NEMC Kanda ya Mashariki Kusini Bw.Hamadi Taimuru akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya ukaguzi kwenye kiwanda bubu cha kukusanya na kusaga chupa za plastiki katika eneo la Kisarawe II wilayani Kigamboni leo Aprili 5,2023 Jijini Dar es Salaam.
**********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limempatia siku saba (7) mmiliki wa kiwanda bubu cha kukusanya na kusaga chupa za plastiki katika eneo la Kisarawe II wilayani Kigamboni kufika katika ofisi za NEMC kujibu tuhuma za kukutwa na taka hatarishi za hospitali katika eneo lake la kiwanda.
Agizo hilo limetolewa leo Aprili 5,2023 Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Utekelezaji wa Sheria NEMC, Bw.Thobias Mwesiga mara baada ya kufanya ukaguzi wa kimazingira na kutembelea na kushuhudia shughuli mbalimbali zinafanyikakwenye kiwanda hicho kinyume na sheria.
Amesema kwa kuwa wamebaini pia kiwanda hicho hakina vibali muhusika huyo atachukuliwa hatua za kisheria kwa kutozwa faini kwa kukiuka taratibu na ataelekezwa utaratibu wa kwenda kusajili kiwanda chake ambacho kinapaswa kusajiliwa kwa mujibu wa sheria.
"Faini itakayotozwa kwa mwenye kiwanda haitakuwa pungufu ya Milioni 5, na faini hiyo ni ya fedha ambayo anailipa kwa serikali". Amesema Bw. Mwesiga.
Aidha NEMC imetoa rai kwa hospitali zote nchini kufuata utaratibu wa namna ya kuteketeza taka zinazotokana na shughuli zao za mahospitalini.
"Sheria za Mazingira na kanuni zake inazitaka hospitali zote nchini kuwa na mfumo na utaratibu mzuri ndani ya hizo hospitali kuteketeza taka zao wenyewe, kuwa na vifaa ambavyo zile taka zinazozalishwa katika hospitali hazitaweza kurudi kwenye mazingira". Amesema
Kwa upande wake Meneja wa NEMC Kanda ya Mashariki Kusini Bw.Hamadi Taimuru amesema watampa maelekezo kwenye kiwanda pindi atakapofika kwenye ofisi za NEMC ndani ya siku saba, na kuanzia sasa wamesimamisha rasmi shughuli zote ambazo zimekuwa zikifanywa kwenye kiwanda hicho mpaka taratibu zote zitakapofuatwa.
"Hii haiwezi kukubarika kwaani hata hawa wanaofanya kazi kwenye kiwanda hiki wanafanya kazi pasipokuwa na vifaa maalumu hivvyo wanaweza kupata na wao madhara kwenye taka hizo za hospitali, madhara kwasasa ni mengi". Amesema Bw.Taimuru.
Pamoja na hayo amesema watahakikisha wanatembelea katika hospitali kuona takataka zao wanazihifadhi na kuzipeleka wapi na kuonesha uthibitisho unaoonesha sehemu ambayo wanazipeleka takataka hizo.
Nae Mmiliki wa Kiwanda hicho, Bw. Salumu Madongo amekiri kuwa kiwanda chake hakina kibali kutoka NEMC lakini vibali vya kiwanda anavyo hivyo basi atafika katika ofisi za NEMC ili aweze kupewa utaratibu na kuweza kupata kibali cha Mazingira.
Kuhusu taka za hospitali kukutwa katika kiwanda chake amesema ni kutokana na wale ambao wanakusanya chupa za plastiki na kuzipeleka pale ndo walikuja na taka hizo zikiwa ndani ya mfuko wa kubebea chupa za plastiki
0 Comments