Ticker

6/recent/ticker-posts

WATU WANNE WAKAMATWA KWA KUCHEZEA VIPIMO KWENYE MADUKA YA KUUZIA NYAMA JIJINI DAR ES SALAAM



************* 

Wakala wa Vipimo Mkoa wa Dar es Salaam imeendeshaukaguzi wa kushtukiza kwenye maduka ya kuuzia nyama kwalengo la kujiridhisha kama Vipimo vinatumika kwa usahihi.Takribani maduka 21 yamekaguliwa na Bucha nne zimebainikakufanya udanganyifu kwa kutokutumia Vipimo kwa usahihi ilikuwapunja wanunuzi wa bidhaa hizo. 

Akizungumza mara baada ya zoezi la ukaguzi wa kushtukizaMeneja wa Wakala wa Vipimo Ilala Bw. Alban Kihullaamesema, kuwa zoezi hilo ni la Kisheria na hufanyika mudawowote, siku yoyote na saa yoyote lengo likiwa ni kuangaliamatumizi ya vipimo kama yanatumika kwa usahihi kwa mujibuwa Sheria. 

Meneja Kihulla amesema, kwa ukaguzi uliofanyikawatuhumiwa wamebainika kuwaibia wateja wao kiasi cha nusukilo katika kila kilo mbili zinazonunuliwa na bucha zinginezimekuwa zikiibia wateja kiasi cha gramu 250 kwenye kila kilo moja ya nyama. 

Kihulla ameeleza kuwa, watuhumiwa wote waliokamatwawamechukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa Sheria ya VipimoSura ya 340 Mapitio ya 2002 na marekebisho yake ili iwe funzokwa wafanyabiashara wengine wenye tabia za kuchezea Vipimo. 

Wakala wa Vipimo inatoa wito kwa Wananchi wote kuwamakini wanapoenda kununua nyama kwenye madukambalimbali na kuwataka washiriki kwenye tukio la upimajikuliko kuwa amini wauzaji na endapo watabaini changamotoyoyote wawasiliane nao kwa namba ya simu ya bila malipo ya0800 110097 kwa msaada. 

Kadharika, wito umetolewa kwa wauzaji wote wa nyamakuachana na tabia za kuvunja Sheria kwa kuwaibia wateja waona wahakikishe wanatenda haki kwa kupima nyama kwa usahihina kwenye mizani sahihi iliyohakikiwa kwani kinyume nakufamya hivyo wataondoa uaminifu kwa wateja wao nawatachukuliwa hatua kali za Kisheria. 

Vilevile, wamiliki wa Bucha za nyama wametakiwa kufuatiliamwenendo wa biashara zinavyofanyika kwenye maeneo yao yabiashara kwa kuwa linapotokea tatizo lolote la wizi kwakutotumia mizani kwa usahihi hawatakuwa salamawatachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa Sheria ya Vipimo.

Post a Comment

0 Comments