Ticker

6/recent/ticker-posts

WATAALAM IDARA BIASHARA NA UWEKEZAJI WA JIJI LA DAR ES SALAAM WANOLEWA


Na Magrethy Katengu, Dar es Salaam

Wataalamu wa Idara Biashara na Uwekezaji Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam wapewa Mafunzo namna bora ya Utekelezaji Majukumu yao katika Idara hiyo mpya iliyoundwa hivi karibuni itakayokuwa ndani ya Sektetarieti Tawala za Mkoa na serikali za Mitaa chini ya Wizara mama ya Uwekezaji Viwanda na Biashara .

Akizungumza leo Jijini Dar es salaam Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Tabu Shaibu wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo hayo yatanayoendeshwa siku kumi na Washiriki wakiwa wachumi na Maafisa Biashara ambapo amewashauri kuhakikisha wanatumia fursa hiyo kuleta matokea chanya ya kiuchumi kwa Nchi .

"Mafunzo haya yamekuja Kwa wakati muafaka kwani waliopo hapa kwenye Mafunzo baada ya miezi 6 kutakuwa na matokeo chanya makubwa katika Jiji letu la Dar es salaam hasa wakati tunapokaa kupanga bajeti zetu "amesema Mkurugenzi

Kwa Upande wake Afisa Biashara Mkuu Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara Amosi Kusaja amesema lengo la Mafunzo hayo ni kushirikiana na Maafisa biashara wa Jiji namna ya ufanyaji kazi zao katika viwango vya juu kwani Dunia Sasa ni biashara na inahitaji ubunifu wa hali ya juu hivyo tutahakikisha tunawapatia Mafunzo kwa kuna wajue Majukumu yao bila kuingiliana kitaasisi .

Naye Mtoa maada Afisa Biashara Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Zabloni Makoye amesema mafisa bishara walio wengi hawafahamu namna na utendaji wa pasipo kuingiliana na taasisi hivyo watapatiwa muongozo wa kuwasaidia wafahamu Mambo mbalimbali ikiwemo manunuzi na Ugavi namna wanapotakiwa kutekeleza kazi zao.

Naye Afisa Masoko Mkuu Wizara Uwekezaji Viwanda na Biashara Ishara Nzamilisi amesema Maafisa Biashara ni daraja kati yao na wazalishaji lakini hapo katikati kumekuwa na madalali wajanja wakitumia fursa ya kujipatia fedha kupitia wazalishaji hivyo Mafunzo hayo watawaelimisha juu ya Masula mazima ya Manunuzi na Ugavi .

Naye miongoni mwa waliopata Mafunzo Afisa Biashara Ally Baruani amesema hapo awali walikuwa wanafanya kazi kama kitengo cha biashara hivyo kupitia kuundwa Idara hiyo mpya itasaidia wao kutatua changamoto zilizokuwa zinawakabili ikiwemo kuwatambua Madalali ambao wamekuwa wakiwanyonya wakulima kwa kuwapangia bei ya mazao hivyo Sasa itawalazimu kuwafuatilia Madalali hao siwanyonye wazalishaji na walipe kodi

Aidha katika Semina hiyo itaendeshwa kwa muda wa siku kumi na Wataalamu wa idara ya Biashara na Uwekezaji kutoka Jiji la Dar es salaam watanufaika na Mafunzo hayo kutoka kwa watoa maada kutoka mbalimbali ikiwemo kutoka Wizara ya Uwekezaji Viwanda Biashara lengo ni Moja kujenga Uwelewa wa kutosha kwa Wataalamu hao.


Post a Comment

0 Comments