Ticker

6/recent/ticker-posts

THAMINI UHAI YATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI KUELEKEA SIKU YA UTEPE MWEUPE

Mratibu wa Muungano wa Utepe Mweupe Tanzania Rose Mlay akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuelekea siku ya Utepe Mweupe inayoadhimishwa Machi 15 ya kila mwaka.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Thamini Uhai Banzi Msumi akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano huo ambapo ametumia nafasi hiyo kueleza wao kama mmoja ya wadau wanaungana na wadau wengine kuelekea siku hiyo.

****************

KATIKA kuelekea Siku ya Utepe Mweupe ambayo huadhimishwa Machi 15 ya kila mwaka, Muungano wa Utepe Mweupe kwa Uzazi Salama(White Ribbon Alliance) umeomba waandishi wa habari nchini kutoa taarifa zinazokwenda sawa nakauli mbiu ya Siku hiyo.

Kauli mbiu ya mwaka huu kwenye Siku ya Utepe Mweupe inaeleza hivi “Kila mwanamke anastahili huduma bora najumuishi za uzazi zenye staha na hesima.

Akizungumza leo Machi 13,2023 kwenye mkutano wawaandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa ofisi zaThamini Uhai jijini Dar es Salaam , Mratibu wa Muungano waUtepe Mweupe Tanzania Rose Mlay amesema katika kuelekea siku hiyo wameamua kukutana na waandishi wa habari wakiwaomba watoe taarifa sahihi kwa lengo la kuisaidia jamii.

“Tumewakumbusha waandishi wa habari katika kuelekea siku hiyo tunawaomba Ombi letu kwa waandishi wa habari watoe habari sawa na kauli mbiu inavyosema kuwa kila mwanamke anastahili huduma bora na jumuishi za uzazi zenye staha na heshima.

“Katika huduma jumuishi tunaona kuna watu hatujawajumuisha kama walemavu wa viungo, akili na wale ambao wako chini ya miaka 18 na wamepata ujauzito. Kwa hiyo tunaomba waandishi waingie mtaani kuzungumza na wale akina mama yaani kwenye jamii.

“Wamama wenye hizi changamoto tunatamani tukiwasikia wakisema wangependa wafanyiwe nini ili wakienda hospitali waridhike na huduma wanazopata na wafurahi kutokana na hali ambazo zinachangamoto kidogo,”amesema Mlay.

Akielezea zaidi siku ya Utepe Mweupe amesema wanatarajia kutakuwa na wadau mbalimbali wakiwemo wananchi, wafanyakazi wa afya na viongozi wa ngazi wa Serikali ili kwa pamoja wajadiliane kuhusu kauli mbiu ya Kila mwanamke anastahili huduma bora na jumuishi za uzazi zenye staha na heshima

“Na ni nini kifanyike ili hata ambao wanachangamoto kama ulemavu yaani kwa pamoja wafanye nini , hivyo tunaomba vyombo vya habari vipeleke hizo habari mpaka ziwafike wananchi wote.”

Mlay ameeleza mbali ya kauli mbiu hiyo kuna mambo ya msingi ambayo yatajadiliwa hasa katika eneo la faragha kwa wanawake wakati wa kujifungua, kuna chumba cha kujifungulia kwa ajili ya faragha ili mjamzito hasa mlemavu au chini yamiaka 18 awe na msindikizaji.

Mengine watakayojadili katika siku hiyo ni Mazingira rafiki yakujifungulia kwa mjamzito mlemavu kwa mfano kitanda nachoo pamoja na vitendo , lugha ya upendo na staha kwa kilamjamzito.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la ThaminiUhai Banzi Msumi amesema katika kuelekea siku hiyo waokama moja ya wadau ambao wako kwenye Muungano wa UtepeMweupe wanaunga mkono uwepo wa siku hiyo.

“Tunaungana na wadau wote katika kuadhimisha siku hiyo yenye kauli mbiu inayosema kila mwanamke anastahili huduma bora na jumuishi za uzazi zenye staha na heshima. Kama kaulimbiu ilivyokaa, Thamini Uhai tunasisitiza zaidi Serikali kuendelea kushirikiana na wadau kutengeneza usiri kwa wanawake wakati wote wa kujifungua.

Pia kuwepo na vyumba ambavyo vitaangalia faragha pamoja na makundi mbalimbali maalumu kama walemavu na akina mama ambao wako chini ya umri wa miaka 18 lakini pia kuweka mazingira rafiki ya kujifungulia kwa wajawazito walemavu kwamfano kitanda na choo kwa ajili ya wamama wenye ulemavu.

“Lakini vitendo pamoja na lugha za staha na upendo kwa kila mjamzito na kama kauli mbiu ilivyokaa na hivi viambatanishi vyake sisi tuko pamoja na siku hii tunayoisubiria kwa furaha sana.”Amesema

Post a Comment

0 Comments