Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu ( katikati) akizindua Programu Dondoo za lishe kwa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi iliyozinduliwa na taasisi ya chakula na Lishe (TFNC), kwa lengo kusaidia kukabiliana na magonjwa nyemelezi na kuimarisha hali zao za lishe, leo Jumatatu machi 06/2023 Jijini Dar es salaam. Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu akizungumza wakati wa uzinduzi wa Programu Dondoo za lishe kwa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi iliyozinduliwa na taasisi ya chakula na Lishe (TFNC) leo Jumatatu machi 06/2023 Jijini Dar es salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt. German Leyna akizungumza wakati wa uzinduzi wa Programu Dondoo za lishe kwa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi iliyozinduliwa na taasisi ya chakula na Lishe (TFNC) leo Jumatatu machi 06/2023 Jijini Dar es salaam. Mwakilishi mkazi wa WFP Nchini Tanzania Sara Gibson akizungumza wakati wa uzinduzi wa Programu Dondoo za lishe kwa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi iliyozinduliwa na taasisi ya chakula na Lishe (TFNC) leo Jumatatu machi 06/2023 Jijini Dar es salaam.Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa taasisi ya chakula na lishe na wageni mbalimbali baada ya kuzindua Programu Dondoo za lishe kwa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi iliyozinduliwa na taasisi ya chakula na Lishe (TFNC) leo Jumatatu machi 06/2023 Jijini Dar es salaam.
**************************************
Serikali kupitia Wizara ya afya imesema kuwa Tanzania imefanikiwa kupunguza viwango vya utapiamlo katika baadhi ya viashara ambapo imebainisha kuwa udumavu umeshuka kutoka asilimia 34 kwa mwaka 2015-2016 hadi asilimia 30 kwa mwaka 2022 kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano.
Hayo yamebainishwa leo Jumatatu Machi 06, 2023 Jijini Dar es salaam na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu wakati wa uzinduzi wa Programu ya Dondoo za lishe kwa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi iliyozinduliwa na taasisi ya chakula na Lishe (TFNC).
Akizungumza wakati akizindua Programu hiyo Pro. Nagu amesema licha ya kupungua kwa takwimu hizo lakini bado kunahitajika kazi ya ziada na kuongeza kasi ili kukabiliana na tatizo la lishe na kukidhi viwango vya kimataifa vya shirika la afya duniani ambapo kiasi kinachpendekezwa hali ya lishe ya udumavu iwe chini ya asilimia 20.
"Lishe hii ni moja ya mikakati ya kuwajengea wananchi uelewa kuhusu masuala ya lishe bora na kuchochea mfumo bora wa lishe,kupitia programu hii naamini Itasaidia kutoa elimu na ujuzi namna ya kuandaa milo na kutumia vyakula vinavyopatikana katika maeneo husika” amesema
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt. German Leyna alisema anaelezea msukumo walioupata hata kutengeneza application hiyo.
"Lengo letu ni elimu ya lishe iwafikie watu wengi nchini ili kila mtu awe na mpangilio mzuri wa mlo wake"
Naye mwakilishi mkazi wa WFP Nchini Tanzania Sara Gibson, alizungumzia ushiriki wao hasa katika kufanikisha application hiyo.
0 Comments