Ticker

6/recent/ticker-posts

TANZANIA NA FINLAND ZAKUBALIANA KUENDELEZA SEKTA YA MISITU NA NYUKI NCHINI.


Na John Mapepele

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa leo Machi 28, 2023 amefanya kikao na ujumbe wa Serikali ya Finland ulioongozwa na Balozi wa Finland hapa nchini, Mhe. Thereza Zitting na kukubaliana uendelezaji na uwekezaji mkubwa kwenye Sekta ya misitu na nyuki hapa nchini.

Mazungumzo hayo yamefanyika ofisini kwake ambapo pande zote mbili zimekubaliana kupitia mikataba ya awali iliyoingiwa na Serikali ya pande zote mbili ili kuiboresha ikizingatiwa kuwa nchi hizi zimekuwa na mahusiano mazuri kwa takribani miaka 40.

Aidha, katika kikao hicho ambacho kilihudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu nchini ( TFS), Prof. Dos Antos Silayo

Amesema Serikali ya Finland imeonyesha nia ya dhati katika uhifadhi wa misitu na kuongeza thamani ya mazao ya misitu na nyuki ili yaweze kuwa katika kiwango cha kimataifa.

Mhe. Mchengerwa amewakaribisha wawekezaji kutoka Finland kuja kuwekeza huku akisisitiza kuwa Tanzania ina maeneo mengi yanayoweza kuwekezwa ambapo Mhe. Balozi Zitting amemhakikishia Mhe waziri kuwaletea wawekezaji hao.

Pia amesema Serikali ya Finland imekuwa ikitoa msaada mkubwa wa mafunzo kwa wananchi kwenye sekta ya Misitu huku akitolea mfano wa Chuo kilichopo Mafinga mkoani Iringa.

Aidha, Mhe. Mchengerwa amesema Serikali ya Finland katika awamu hii imekubali kuisaidia Tanzania vifaa katika kukabiliana na majanga kwenye Maeneo ya misitu yaliyohifadhiwa kama moto na ujangili.

Post a Comment

0 Comments