Wafanyakazi wanawake wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma, wakiwa wamejipanga tayari kwa maandamano katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika ngazi ya Mkoa, wilayani Kondoa mkoani Dodoma, maadhimisho hayo yenye kauli mbiu “Ubunifu na Mabadiliko ya Teknolojia Chachu katika kuleta Usawa wa Kijinsia”.
Wafanyakazi wanawake wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma, wakiwa katika maandamano walipoungana na wanawake duniani kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ambapo ngazi ya mkoa Dodoma yamefanyika wilayani Kondoa maadhimisho hayo yenye kauli mbiu “Ubunifu na Mabadiliko ya Teknolojia Chachu katika kuleta Usawa wa Kijinsia”yamefanyika katika Wilaya ya Kondoa.
Wafanyakazi wanawake wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma, wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kushiriki maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambapo ngazi ya mkoa Dodoma yamefanyika wilayani Kondoa maadhimisho hayo yenye kauli mbiu “Ubunifu na Mabadiliko ya Teknolojia Chachu katika kuleta Usawa wa Kijinsia”yamefanyika katika Wilaya ya Kondoa.
Wafanyakazi wanawake wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma,wakipanda miti katika kituo cha afya Mkonze,katika kuadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani .
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Dodoma Mhandisi Donasiano Shamba akiwaunga mkono wanawake wa Shirika katika kupanda miti kwenye kituo cha afya Mkonze.
Wafanyakazi wanawake wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma,wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kupanda miti 200 katika kituo cha afya Mkonze,katika kuadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani .
Na.Alex Sonna-DODOMA
Wafanyakazi wanawake wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma, wameadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa kuungana na wanawake wengine kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali na Binafsi katika maadhimisho hayo ngazi ya Mkoa, wilayani Kondoa.
Maadhimisho hayo yamefanyika leo ambapo Mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt Rosemary Senyamule, Wanawake wa TANESCO Dodoma kama sehemu ya maadhisho haya wameweza kuigusa jamii kwa kuchangia upandaji miti kupitia Kampeni ya Shirika hilo ya kutunza Mazingira.
Akizungumzia ushiriki wa TANESCO Dodoma katika Maadhimisho hayo, Afisa Rasilimali watu na Mwakilishi wa Wanawake Mkoani Dodoma Bi.Stephanie Nandy, amesema mwaka huu kama Shirika tumeadhimisha kwa kupanda miti 200 katika kituo cha afya Mkonze, ikiwa ni sehemu ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi.
Bi.Nandy amesema wameamua kupanda miti kwa kuwa uzalishaji Umeme unategemea sana mvua inayotokana na miti na utunzaji wa Mazingira, hivyo zoezi hilo litasaidia kukabiliana na athari za kimazingira na hatimaye mvua za kutosha kunyesha.
''Kupitia Kampeni yetu, tumepanda miti 200 ya matunda ya aina mbalimbali ikiwemo Michungwa, Miembe, Miparachichi na Mipera katika eneo la Kituo cha Afya cha Mkonze Jijini Dodoma ili kufanikisha malengo yetu ya kimazingira kupitia kauli mbiu ya Shirika ya PANDA MITI, MAJI NDI, UMEME NDINDINDI!!" amesema Nandy
Pia aliongeza kuwa imekuwa siku nzuri kwao kukutana wanawake kwa pamoja ili kuadhimisha siku hiyo Muhimu ambapo Wanawake wamesisitizwa Ubunifu kuelekea maendeleo zaidi.
Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa Mwaka huu ni Ubunifu na Mabadiliko ya Teknolojia Chachu katika kuleta Usawa wa Kijinsia.
0 Comments