Ticker

6/recent/ticker-posts

TAASISI ZATAKIWA KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZA UTEKELEZAJI SHERIA YA MAZINGIRA


Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Andrew Komba akifungua Warsha ya Kupitia Taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji na Changamoto za Mfumo wa Kitaasisi na Kisheria wa EMA nchini kwa niaba ya Katibu Mkuu iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma.

Washiriki wakiwa katika Warsha ya Kupitia Taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji na Changamoto za Mfumo wa Kitaasisi na Kisheria wa EMA nchini iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma.


Mratibu wa Mradi wa Kuimarisha Uwezo wa Kitaasisi wa Utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira (EMA) Bw. Richard Masesa akitoa neon la utangulizi wakati wa Warsha ya Kupitia Taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji na Changamoto za Mfumo wa Kitaasisi na Kisheria wa EMA nchini iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma.


Washiriki wakiwa wa Warsha ya Kupitia Taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji na Changamoto za Mfumo wa Kitaasisi na Kisheria wa EMA wakiwa katika picha ya pamoja.

********************

Ofisi ya Makamu wa Rais imetoa wito kwa taasisi zinazowajibika na utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira (EMA) ya mwaka 2004 zimetakiwa kushughulikia changamoto za utekelezaji wake.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Andrew Komba wakati akifungua Warsha ya Kupitia Taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji na Changamoto za Mfumo wa Kitaasisi na Kisheria wa EMA nchini.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Komba amesema Serikali ya Tanzania ilichukua hatua ya kulinda na kuhifadhi mazingira kwa kuweka Sera ya Taifa ya Mazingira (1997) na Sheria ya Usimamizi wa Mazingira (EMA) (2004).

Amesema Sheria hiyo imeweka mfumo wa kiutawala na kitaasisi wa usimamizi wa mazingira unaojumuisha ngazi zote za kiutawala katika Serikali unaojumuisha Wizara na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

“Ndugu zangu washiriki wa warsha hii licha ya juhudi za Serikali za kusimamia uhifadhi na wa mazingira, bado kuna changamoto na upungufu katika taasisi zinazowajibika utekelezaji wa Sheria ya Mazingirakamili wa EMA.

“Hivyo, katika warsha hii mtapitia rasimu ya taarifa ya tathmini ya utekelezaji na changamoto za mfumo wa kitaasisi na kisheria uliopo wa usimamizi wa mazingira nchini,” amesema Dkt. Komba.

Ameongeza kuwa maoni kuhusu tathmini juu ya utekelezaji na changamoto za mfumo uliopo wa kitaasisi na kisheria wa usimamizi wa mazingira utatoa matokeo muhimu ya kuimarisha utekelezaji wa EMA kupitia upungufu uliobainishwa.

Aidha, Mkurugenzi huyo amelipongeza na kulishukuru Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) kwa juhudi zake katika kushirika kuimarisha uwezo wa Taifa wa utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira kupitia Mradi wa Kuimarisha Uwezo wa Kitaasisi wa Utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira (EMA).

Post a Comment

0 Comments