TAARIFA ZAIDI KUTOKA JESHI LA POLISI TANZANIA KUHUSU KIFO CHA ANAYESHUKIWA KUWA MCHIMBAJI HARAMU
Dar es Salaam, Tanzania, Machi 21, 2023 – Kampuni ya Dhahabu ya Barrick (NYSE:GOLD) (TSX:ABX) – Kama ilivyoripotiwa mnamo tarehe 12 Machi 2023, tukio lihusianalo na usalama lilitokea katika Mgodi wa Dhahabu wa North Mara (NMGM) mnamo Machi 11, 2023 na kusababisha kifo. Kikifanyia kazi taarifa zilizopokelewa, kikosikazi huru cha Serikali ya Tanzania kinachopambana na utoroshwaji wa dhahabu kiliomba kuingia kwenye mgodi wa North Mara ili kukagua eneo lililokuwa na vizuizi katika sehemu ya mgodi wa chini kwa chini, ambapo palishukiwa kuwa uchimbaji haramu ulikuwa ukifanyika.
Kufuatia ukaguzi huo, mchimbaji haramu alipatikana katika chimbo lisilotumika na lililokuwa limezungushiwa kizuizi na, katika harakati za kujaribu kutoroka asikamatwe, alianguka na kufariki. Jeshi la Polisi lilianzisha uchunguzi rasmi wa tukio hilo na kutoa taarifa kuwa aliyefariki ni Emmanuel Chacha, mfanyakazi wa NMGM na kuwa taarifa kamili ya tukio hilo itatolewa baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa mwili wa marehemu.
Katika taarifa yake iliyotolewa Machi 20, 2023, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kanda Maalumu ya Kipolisi ya Tarime-Rorya, ACP (Kamishina Msaidizi wa Polisi) Geofrey Sarakikya, alithibitisha kuwa taarifa zilizopatikana kutoka kwa watu waliokuwapo eneo la tukio pamoja na matokeo ya uchunguzi wa mwili wa marehemu, kifo cha marehemu kilitokana na majeraha yaliyosababishwa na kuanguka kutoka juu.
Wakati wa uchunguzi huo, kulikuwa na taarifa za uvumi kwenye mitandao ya kijamii, zikidai kuwa Bw. Chacha alikufa kwa kupigwa risasi, zikitaka kuyumbisha uchunguzi wa polisi unaoendelea. Katika maelezo yake, Kamanda wa Polisi Mkoa alithibitisha kuwa taarifa hizo hazina ukweli. Vitendo kama hivyo si tu kwamba havisaidii, bali pia vinaonesha ukosefu wa hali ya juu wa uwajibikaji kwa vile vinachochea na kuhimiza uvumi kabla ukweli wote haujathibitishwa na uchunguzi kufuata hatua stahiki.

Kwa maelezo zaidi kutoka Barrick
Mahusiano ya Kampuni na wawekezaji na vyombo vya habari
Kathy du Plessis
+44 20 7557 7738
+27 83 266 5847
Baruapepe: barrick@dpapr.com
Meneja wa nchi wa Mawasiliano na uhusiano wa Kampuni
Georgia Mutagahywa
+255 754 711 215
Baruapepe: georgia.mutagahywa@barrick.com
Tovuti: www.barrick.com
05089-00004/13965852.1
0 Comments