Ticker

6/recent/ticker-posts

SIMBA SC YAZIDI KUTAMBA KIMATAIFA, YAICHAPA VIPERS


NA MWANDISHI WETU 

WAWAKILISHI Katika Michuano ya Klabu Bingwa Afrika timu ya Simba SC imejiweka katika mazingira mazuri ya kutinga Robo Fainali ya Michuano hiyo baada ya kuichpa bao 1-0 Vipers Mchezo wa Kundi C uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. 

Wenyeji walipata bao la kwanza dakika ya 45 likifungwa na Clatous Chama akimalizia pasi ya Moses Phiri na kuipeleka Simba mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0 dhidi ya Vipers. 

Kwa ushindi huo Simba imefikisha Pointi 6 katika nafasi ya pili na kujiweka nafasi nzuri ya kutinga robo baada ya wapinzani wao wa karibu Timu ya Horoya kupoteza mchezo wake dhidi ya Vinara Raja Casablanca wenyeji Pointi 12,Horoya inashika nafasi ya tatu wakiwa na Pointi 4 huku Vipers ikishika mkia wakiwa na Pointi 1. 

Sasa Simba ili iweze kutinga Robo Fainali inahitaji kupata ushindi katika mchezo wake dhidi ya Horoya Mchezo utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa Machi 17 au 18 mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments