Ticker

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YAJA NA MFUMO WA MSHITIRI UPATIKANAJI WA BIDHAA ZA AFYA

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Mhe.George Mmbaga akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wawezeshaji wa mfumo wa Mshitiri ambayo yamefanyika leo Machi 23,2023 mkoani Tanga.
Wawezeshaji wa mfumo wa Mshitiri Mkoa wa Tanga.


**************************


Na Hamida Kamchalla, TANGA.

KATIKA uboreshaji wa huduma za afya serikali imekuwa ikitekeleza afua mbalimbali ili kuhalikisha upatikanaji wa bidhaa za afya unakuwa asilimia 100 ikiwemo mfumo wa Mshitiri.


Uwepo wa mfumo huo ni utekelezaji wa ilani ya Ccm ya uchaguzi, ambao unawezesha upatikanaji wa bidhaa za afya ambazo zinakosekana katika Bohari ya Dawa (MSD), hivyo kuimarisha na kurahisisha vituo vyote vya kutolea huduma za afya nchini.


Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Georde Mmbaga ameyasema hayo leo Machi 22,2023 wakati akizindua mafunzo ya wawezeshaji wa mfumo wa Mshitiri mkoani humo, ambao akieleza kwamba lengo la mafunzo hayo ni kupata wawezeshaji wa Mkoa na halmashauri za wilaya wa mfumo huo.


"Upatikanaji wa dawa na vipimo vya kitabibu kwa uhakika katika kituo cha huduma, kwa kiasi kikubwa unaakisi ubora wa huduma zinazotolewa mahali husika, kwa kulitambua hilo, serikali yetu imekuwa ikitekeleza afua mbalimbali ili kuhalikisha upatikanaji wa bidhaa za afya unakuwa kwa asilimia 100, ikiwemo mfumo huu wa Mshitiri " amesema.


"Sisi kama viongozi, tuna jukumu la kuvisimamia vituo ili viweze kukusanya mapato ya kutosha kwa ajili ya ununuzi wa bidhaa za afya, sambamba na kusimamia mnyororo wa ugavi wa bidhaa hizo,


"Kwa kutekeleza haya, watu wote watapata huduma za bidhaa za afya katika vituo vyetu vya kutolea huduma za afya bila manung'uniko, hasa tunapoelekea katika utekelezaji wa bima ya afya kwa wote" ameeleza.


Aidha Mmbaga amebainisha kwamba katika mafunzo hayo washiriki ambao ni wahudumu wa afya watajifunza utekelezaji wa mfumo wa Mshitiri kwa kupitia mwongizo wa utekelezaji wa mfumo huo pamoja na mfumo wa kielektroniki wa usimamizi wa taarifa.


"Ili mfumo wa Mshitiri uweze kuwa thabiti, tunatakiwa kusimamia vizuri kuanzia utaratibu wa awali wa upatikanaji wa Washitiri hadi utekelezaji wa katiba, nina imani kupitia mafunzo haya , sote tutaondoka na uelewa wa pamoja wa utekelezaji wa mwongozo wa mfumo huu" amesema.


Pia Mmbaga amesisitiza, "tukasimamie ukusanyaji wa mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya, ili viweze kulipa Washitiri kwa wakati mara baada ya kupokea shehena ya bidhaa, na kuepusha madeni yasiyo ya lazima" aliongeza.


Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dr. Rehema Majid mesema mafunzo hayo yameshirikisha halmashauri zote za Mkoa na kupitia mfumo huo hakutakuwa na upungufu wa bidhaa za afya na kwamba utaondoa malalamiko ya wananchi katika vituo vya kutolea huduma za afya.


"Washiriki wa mafunzo haya ni wakurugenzi, waganga wakuu wa halmashauri, wataalamu wa maabara, tehama na wafamasia, kutoka katika halmashauri zote 11 za Mkoa wa Tanga, hawa ndio watakaokwenda kuwafunsha wenzao katika vituo husika" amesema.


"Mfumo ni mzuri sana kwa sababu, endapo MSD ikikaukiwa basi makampuni yatakayoingia katika Mshitiri yatahakikisha dawa au vifaa vinakuwepo muda wote katika vituo, tutapunguza manung'uniko ya wananchi kukosa baadhi ya huduma wanapokwenda kupata tiba" amesisitiza.


Washiriki wa mafunzo hayo wmesema mfumo huo utakwenda kuwarahishia katika utendaji wao kwakuwa watafanya kidigitali na kuondokana na ule mfumo wa zamani wa kutumia makaratasi.

Post a Comment

0 Comments